Milk Crate Challenge: Mchezo utakaowapa wengi majeraha na ulemavu wa kudumu

Milk Crate Challenge: Mchezo utakaowapa wengi majeraha na ulemavu wa kudumu

The Sheriff

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2019
Posts
747
Reaction score
2,112
Milk-Crate-Challenge.png

Huu mchezo unaoitwa Crate Challenge ambao video zake zimeshika kasi katika mitandao ya kijamii hususan Tik Tok na Instagram huenda, kabla haujapoteza umaarufu wake, ukawaacha watu wengi na majeraha makubwa au pengine ulemavu wa kudumu.

Video nyingi nilizopata kuona zinaaashiria mchezo huu unafanyika zaidi Marekani na huenda umeanza kuigwa au labda unaelekea kuigwa maeneo mengine duniani. Sina hakika.

Kinachofanyika ni kreti za chupa za maziwa (za huko kwao) kupangwa kutengeneza umbo linalofanania ngazi za kupanda ghorofani (staircase), ambazo nyingi nimeona zikiundwa kwa urefu wa ngazi (steps) 7. Kreti hizi hazionekani kuwa imara na thabiti kama hizi za bia na soda ambazo tumezoea kuziona huku kwetu.

Hivyo basi, anachotakiwa kufanya mshiriki ni kukwea ngazi hizo mpaka juu na kisha kushukia upande wa pili. Kufanya hivyo bila kudondoka ndio ushindi, jambo ambalo si wengi wanafanikiwa. Wengi hudondoka vibaya hadi kuhitaji huduma za dharura.

Hata hivyo kuna ambao wanafanya mchezo huu kuonekana a piece of cake. Wanapanda na kushuka bila kuanguka.

Wapo wanaoshiriki mchezo huu kwa ajili ya pesa na wengine kama burudani na kuonesha umahiri wao. Wenyewe wanasema ni Hood Olympics.

Nilipata kujua mchezo huu kupitia Snoop Dogg kwakuwa ninaufuata ukurasa wake wa Instagram. Baadaye nikavutiwa kuifuata hashtag ya hiyo challenge ili nipate uhondo wa kutosha. Zipo zilizonichekesha lakini pia zipo zilizonifanya nikasema, ouch!

Nasema hivi, by the time huu mchezo una-expire, utakuwa umegharimu watu wengi viungo vyao kwa namna tofauti.

Kwa sasa tuendelee kula burudani ila nisingependa tuige hii.

It’s all fun a games until… (malizia)






HAWA NI BAADHI YA WALIOFAULU HII "CHALLENGE"






HUYU, INASEMEKANA, DIDN'T MAKE IT

 
Sorry mkuu ouch ni nini?

Kihisishi flan hivi vile vineno vya kiswahili kama toba..au mtu akikuumiza vile ukijigonga kwenye pembe ya kitanda haaf kidole cha mwisho ungekuwa mzungu ungesema ouch[emoji23][emoji23][emoji23] au son of a b**tch
 
Kihisishi flan hivi vile vineno vya kiswahili kama toba..au mtu akikuumiza vile ukijigonga kwenye pembe ya kitanda haaf kidole cha mwisho ungekuwa mzungu ungesema ouch[emoji23][emoji23][emoji23] au son of a b**tch
Ahsante sana kwa kunisaidia kumuelewesha Hornet.
 
Back
Top Bottom