- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Dkt. Bashiru Ally ni mbunge wa kuteuliwa wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. Bashiru amewahi kuwa katibu mkuu wa wa chama cha mapinduzi (CCM) 2018-2021 na katibu mkuu kiongozi.
Madai
Ipo grafiki inayosambazwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiwemo Facebook inayoonekana kuwa na utambulisho wa chombo cha habari cha Millard Ayo ikiwa na ujumbe unaosomka
"BASHIRU AMKANA POLEPOLE NA VIBARAKA WAKE"
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao na utafutaji wa maneno muhimu umebaini kuwa hakuna chanzo cha kuaminika kilichochapisha taarifa hiyo katika mitandao ya kijamii.
Taarifa hiyo pia haijachapishwa na Millard Ayo kama inavyoonekana. Grafiki hiyo haijachapishwa na chanzo hicho na badala yake ni ya kughushi.
Taarifa hii imekuw ani muendelezo wa upotoshaji unaofanyika tokea kipindi ambacho Balozi Humphrey Polepole alipotangaza kujiuzulu nafasi yake ya Ubalozi wa Tanzania nchini Cuba Julai 13, 2025.