SI KWELI PreGE2025 Millard Ayo amechapisha taarifa ikisema "CHADEMA iko kipindi cha kupotea kisiasa"

SI KWELI PreGE2025 Millard Ayo amechapisha taarifa ikisema "CHADEMA iko kipindi cha kupotea kisiasa"

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
MILARD_SIKWELI9JUN25.jpg
 
Tunachokijua
Maria Sarungi ni mwanaharakati kutoka nchini Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia.

Kadhalika Maria amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali ya harakati za kisiasa kwa kipindi kirefu sasa, ambapo amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuendsha harakati zake ikiwemo X awali ukijulikana kama twitter kwa sasa akiipigia chapuo kampeni ya No reforms, no election ya CHADEMA inayodai mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuchochea uhuru, haki na uwazi.


Taarifa inayomhusisha Maria Sarungi dhidi ya CHADEMA
Ipo taarifa iliyochapishwa katika mtandao wa Facebook kuwa Maria Sarungi ameweka ujumbe kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X akisema CHADEMA iko kwenye kipindi cha kupotea kabisa kisiasa ambapo ujumbe huo unaonekana kunukuliwa kupitia chapisho la Millard Ayo.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search), uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani Ujumbe huo haujachapishwa na Maria Sarungi bali umetengenezwa na wapotoshaji.

Vilevile chapisho lililotumika kusambaza taarifa hiyo ni la kughushi kwani halijachapishwa na Millard Ayo bali limetumia utambulisho huo ili kupotosha.

Hivyo ni muhimu kuthibitisha uhalisia wa machapisho yanayosambazwa mtandaoni ili kuepuka kuamini na kusambaza taarifa zisizo za kweli kwani zinaweza kuchochea maamuzi yasiyo sahihi kwa wananchi.​
Back
Top Bottom