- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Wakuu hii taarifa nimekutana nayo Facebook je, ni ya kweli?
ππππ πππ πππππππππ πππ πππ ππ πππππππππ πππππππ πππππ ππ πππππ
Habari za ndani kabisa ya CHADEMA zinasema bundi ameendelea kulia; safari hii Boni Yai akitajwa kuwa mbioni kujiuzulu kutoka nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho Kanda ya Pwani, na kwamba barua yake ya kujiuzulu tayari ameshaiwasilisha kwa Katibu Mkuu John Mnyika.
Hatua hii inatokana na kutokukubaliana na uongozi mbovu wa Tundu Lissu na migogoro inayoendelea ndani ya chama hicho.
Kujiuzulu kwa Boni Yai kunadhihirisha mpasuko mkali ndani ya CHADEMA, huku migawanyiko ya kimtazamo ikizidi kuleta mvutano mkubwa kati ya wanachama na viongozi wa juu wa chama.

- Tunachokijua
- Boniphace Jacob (Boni Yai) ni mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kanda ya Pwani lakini pia amewahi kuwa Meya wa Kinondoni.
Mara kadhaa kumekuwapo taarifa za upotoshaji ambazo zimekuwa zikitaja uwepo wa migogoro ndani ya CHADEMA huku zikiwahusisha viongozi mbalimbali wa chama hicho. rejea hapa, hapa na hapa.
Hata hivyo mnamo Februari 18, 2025 mmoja wa makada wa chama hicho, Lembrus Mchome aliwasilisha pingamizi la kupinga uteuzi wa viongozi watendaji wa juu wa sekretarieti na wajumbe wa kamati kuu ya chama hicho uliofanywa na Mwenyekiti Tundu Lissu Januari 22, 2025 akidai kuwa umekiuka katiba ya chama hicho.
Aidha mnamo tarehe 21, Februari 2025 kupitia mtando wa facebook iliibuka taarifa iliyokuwa ikisambazwa katika mtandao huo kuwa mwandishi wa habari Millard Ayo alichapisha taarifa yenye kichwa cha habari 'Boni Yai kujiuzulu uenyekiti CHADEMA kanda ya pwani'
Pia Boniphace anadaiwa kuwa amesema "Lissu anawakwamisha wagombea wa Chadema kwa kauli ya 'No Reform, No Election,' ikizua taharuki kuhusu uwezo wa chama kuandaa wagombea."
Je, uhalisia upoje?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia maneno muhimu (KeyWordSearch) umebaini kuwa Taarifa hiyo Si ya Kweli, na haijachapishwa na Millard Ayo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.
Aidha nukuu inayoambatanishwa na chapisho lenye taarifa hiyo kuwa Boniphace amesema Lissu anakwamisha wagombea kwa kauli ya 'No Reforms No Election' si ya kweli kwani hakuitoa mahali popote bali imetengenezwa na wapotoshaji kwa lengo la kupotosha.
Kuhusu madai ya kuwasilisha barua ya kutaka kujiuzulu katika nafasi ya unyekiti kanda ya pwani ndani ya chama hicho si ya kweli kwani katibu mkuu wa chama hicho John Mnyika hajathibitisha kupokea barua hiyo.