- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
JamiiCheck tafadhali mtusaidie kupata uhalisia wa hii
=====
πππππ πππππππ : πππππππ πππππππππ ππππππ ππππππππ ππππ ππ 2025
Mwanaharakati Maria Sarungi ametoa maoni makali kuhusu mustakabali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025. Kupitia mtandao wa X (zamani Twitter), ameeleza kuwa chama hicho kimekosa umoja na mipango thabiti, hali inayopelekea migogoro ya mara kwa mara na kukosekana kwa uongozi imara ndani ya chama.
Kwa mujibu wa Sarungi, CHADEMA inakabiliwa na changamoto kubwa za ndani ambazo zinaweza kuathiri nafasi yao katika uchaguzi ujao. Aidha, ametaja kuwa mgawanyiko wa uongozi na kushindwa kuimarisha mshikamano wa wanachama wake ni dalili za kushindwa vibaya katika uchaguzi wa 2025.

- Tunachokijua
- Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia. Maria amekuwa akijihusisha na masuala mbalimbali ya siasa kwa kipindi kirefu sasa, amekuwa akitumia mitandao ya kijamii kuendsha harakati zake ikiwemo X awali ikijulikana kama twitter.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA ) ni chama cha siasa nchini Tanzania kikiwa ni chama kikuu cha upinzani. Mara baada ya uchaguzi mkuu ndani ya chama hicho uliofanyika Januari 21, 2025 zimekuwepo taarifa potoshi kuhusu CHADEMA, tazama hapa, hapa, hapa na hapa.
Kumekuwapo na taarifa inayosambaa mtandaoni inayodaiwa kuchapishwa na Millard Ayo ambayo inamnukuu Maria Sarungi kuwa amesema CHADEMA inakabiliwa na migogoro hivyo kuashiria kushindwa katika uchaguzi mkuu 2025.
Je, ni upi uhalisia wa chapisho hilo?
Ufuatiliaaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia Google reverse image search ulibaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishwa na Millard Ayo kupitia kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.
Aidha chapisho hilo lilitengenezwa kwa kutumia utambulisho na alama za Millard Ayo ili kusambaza taarifa isiyo ya kweli kwani Sarungi hakuchapisha taarifa iliyohusu uwepo wa migogoro na ukosefu wa uongozi imara ndani ya CHADEMA katika ukurasa wake wa mtandao wa X Februari 04, 2025 kama inavyoonekana katika taarifa hiyo.
Hata hivyo JamiiCheck imebaini mapungufu kadhaa yanayoitofautisha taarifa hiyo na taarifa ambazo hutolewa na Millard, sehemu ya mapungufu hayo ni pamoja na kutofautiana kwa muundo wa kuunanisha picha mbili katika chapisho moja, kutokuwepo kwa chapa ya nembo (watermark) ya Millard Ayo.