SI KWELI Millard Ayo amechapisha taarifa inayosema Lissu adai wanawake ni dhaifu sana

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Wakuu wa JamiiCheck ni kweli Millard Ayo amechapisha taarifa inayosema Lissu adai wanawake ni dhaifu sana?

 
Tunachokijua
Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika kila ifikapo Machi 08 ya kila mwaka ambapo wanawake katika mataifa mbalimbali hutumia siku hiyo kusheherekea mafanikio waliyoyapata katika nyanja mbalimbali kama siasa, uchumi, tamaduni na kadhalika.

Kwa mwaka 2025 nchini Tanzania maadhimisho hayo yalifanyika kitaifa jijini Arusha huku mgeni rasmi akiwa ni Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha Baraza la Wanawake Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) BAWACHA liliadhimisha siku hiyo jijini Dar es salaam, katika ukumbi wa Mlimani City ambapo mgeni rasmi alikuwa ni mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu.

Madai yaliyoibuka mtandaoni

Kumekuwapo na taarifa yenye tarehe 08 Mwezi Machi 2025 ikirejea siku ya wanawake, inayodaiwa kuchapishwa na Millard Ayo ikiwa na kichwa cha habari kinachosema ' Lissu adai wanawake ni dhaifu sana'


Uhalisia wa madai hayo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck uliohusisha utafutaji wa kimtandao kwa kutumia maneno muhimu (Key Word Search) ulibaini kuwa Chapisho hilo halikuchapishwa na Millard Ayo katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii kama inavyoonekana.

Aidha taarifa hiyo si ya kweli kwani Tundu Lissu hakutoa kauli kauli hiyo bali katika hotuba yake alisisitiza umuhimu wa mabadiliko ya mifumo ya kisiasa hasa kupitia chaguzi ili kuimarisha usawa bila kujali jinsia katika ushiriki wa masuala ya uchaguzi nchini.

Pia alibainisha maeneo mbalimbali ambayo yamekuwa na hali isiyokuwa na usawa wa kijinsia baina ya wanawake na wanaume ikiwemo elimu, ajira, uchumi, siasa ambapo alisema ili kuleta usawa ni lazima wanawake washiriki kikamilifu katika kupambania mabadiliko muhimu ya kisiasa yatakayowesha na kuinua usawa kwa wote.

View: https://www.youtube.com/live/BhVRj5tp_z8?si=BAdsUpIH8PNDg63W&t=19318
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…