Millya: Tanzania itaendelea kutekeleza wajibu wake mkuu wa kusukuma juhudi za kuanzishwa EAC

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, James Ole Millya amesema Tanzania ikiwa mwanachama mwaminifu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), itaendelea kutekeleza wajibu wake mkuu wa kusukuma juhudi za mtangamano ili kufikia malengo ya kuanzishwa kwa jumuiya hiyo.

Amesema hayo leo Jumatatu, Aprili 13, 2026 baada ya kuapishwa katika Bunge la Jumuiya ya Mashariki (Eala), jijini Arusha na Spika wa Bunge hilo, Joseph Ntakirutimana.

Millya ambaye pia ni Mbunge wa Simanjiro amesema Waziri wa Mambo Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, Balozi Thabit Kombo anaamini ushirikiano wa nchi wanachama ni nguzo muhimu katika kukuza malengo ya kuanzishwa EAC.

“Mtakumbuka kabla kushika nafasi hii (ya naibu waziri) nilikuwa mbunge wa Bunge hili ambalo nilifurahi kufanya kazi pamoja nanyi, nimefurahi kurudi tena na ninaahidi nitajitolea kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha tunakuwa na jumuiya bora na ninatambua umuhimu wa Bunge hili maalumu, ninaahidi kutimizia wajibu wangu wa kuhakikisha Eala inakuwa chombo cha kusimamia ajenda ya mtangamano,” amesema Millya.

Screenshot 2026-04-13 174852.png
 
View attachment 3572128
well done waziri
 
Back
Top Bottom