mimba changa

korino

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2011
Posts
1,004
Reaction score
666
habari zenu wanajf! nlipata ujauzito lkn ukaharibika miez mitatu iliyopita..(ilitoka kwasababu nlitumia dawa za malaria ikiwa nna mimba ila nlikuwa cjajijua km nna mimba)na sasa nimekamata tena mimba je ni mambo gani yakuzingatia ktk utunzaji wa mimba isiharibike na je ni vyakula gani muhimu kuvila kwa muda huu wa mimba ikiwa changa!? maana naogopa hata kufanya shuhuli za nyumban km kupiga deki,kufua n.k nahis inaweza ikatoka! nisaidieni ndugu zangu
 
pole sana bibie, cha msingi utambue kwamba mimba iliyo chini ya miezi 5 iko hatarini sana kudhurika na kemikali chache tuzipatazo kwenye milo yetu each day.

pendelea kula mboga mboga, matunda tofauti, mayai( hususani ya kienyeji), samaki au dagaa wa maji baridi( ziwani) kwa sababu wa baharini wana mercury nyingi ambayo si nzuri wakati una kiumbe ndani.

usipendelee kula maini, kwa sababu maini ndiyo yanayopambana na sumu mwilini, hivyo mabaki ya sumu katika maini ya wanyama yaweza yakawa sumu mwilini, ukila nyama hakikisha imeiva vizuri.

EPUKA VINYAJI KAMA CHAI, KAHAWA, POMBE NA VINGINEVYO AMBAVYO HUCHANGAMSHA.


naishia hapa, wengine waja!!!
 
shukran sana ndugu yangu nitafanya hivyo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…