Mimba changa

Mimba changa

Kifai

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
816
Reaction score
173
Jamani wana jamii forum hbr gani? Shemeji yenu amekuwa anatapika cku nzima ana mimba ya miezi 2 ila inamsumbua mno, jamani anaweza ku2mia dawa gani?
 
Aogee maji ya ziwani kwa siku 3 then alale kuelekea kusini mashariki mwa kitanda.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Aogee maji ya ziwani kwa siku 3 then alale kuelekea kusini mashariki mwa kitanda.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
mmmmh, ushauri wako unanitisha
 
mpeleke hospital haraka, ikiwezekana kwa specialist wa wamama....
 
Avumilie tu.
Hiyo ni hali ya kawaida. Kwa kimombo wanaitwa 'morning sickness'. Atajisikia hali hiyo mpaka mimba itakapokuwa na miezi 4 ndio inakomaa. Ila kutapika hasahasa ni muda wa asubuhi. Kama yeye anatapika siku nzima, mpeleke akaonane na daktari. Huenda kukawa na ushauri afanye nini.
 
Mie bwana mie acheni tu. Morning sickness si lazima iwe asubuhi, inaweza kuwa muda wowote manake mi hata usiku nilikuwa natapika na nilitapika mpaka siku najifungua.
Huyo mpendwa wetu apendelee kunywa chai ya tangawizi. Yaani achemshe tangawizi mbichi kwenye maji anywe kabla hajatoka kitandani. Ahakikishe hakai na njaa hata kidogo na akitapika ale tena havitokagi vyote. Apendelee kunywa fluids nyingi kama natural juices, supu, maji,uji, maziwa.... Pia kuna dawa inaitwa NOSIC. Kuna ambao huwa inawasaidia. Mie kwa kweli ninazo mpaka leo hazikunisaidia. Mwenyezi Mungu atamjaalia wepesi na atalea mimba yake na atajifungua salama tu. Mie toto langu lilikuwa 4 kgs pamoja na kutapika huko kote.
 
Hairuhusiwi mjamzito kunywa dawa yoyote isipokua kwa ushauri wa daktari,mimba changa zinasumbua sana mpaka ikifika miezi minne ila inategemea na mtu.
 
kama anatapika sana na ni mfululizo inaweza kuwa hyperemesis gravidarum, sijui kiswahili chake, anaweza kutumia dawa ya kuzuia kutapika ila inabd daktari amuone sio lazima awe daktari mtaalam wa wanawake...pia tangawizi imethibitishwa kisayansi kusaidia kuondoa kutapika kwa wajawazito, unaweza ku google MORNING SICKNESS AND GINGER, so unaweza mshauri atumie tangawizi itamsaidia
 
Back
Top Bottom