Mie bwana mie acheni tu. Morning sickness si lazima iwe asubuhi, inaweza kuwa muda wowote manake mi hata usiku nilikuwa natapika na nilitapika mpaka siku najifungua.
Huyo mpendwa wetu apendelee kunywa chai ya tangawizi. Yaani achemshe tangawizi mbichi kwenye maji anywe kabla hajatoka kitandani. Ahakikishe hakai na njaa hata kidogo na akitapika ale tena havitokagi vyote. Apendelee kunywa fluids nyingi kama natural juices, supu, maji,uji, maziwa.... Pia kuna dawa inaitwa NOSIC. Kuna ambao huwa inawasaidia. Mie kwa kweli ninazo mpaka leo hazikunisaidia. Mwenyezi Mungu atamjaalia wepesi na atalea mimba yake na atajifungua salama tu. Mie toto langu lilikuwa 4 kgs pamoja na kutapika huko kote.