mm nakushauri msitoe mimba hiyo, bali hakikisha mke wako anahuduria clinic zote na aeleze kuwa mtoto wa awali alizaliwa kwa operesheni tarhe......... ili apate special medical attetion/services.
Sababu zinazonisukuma kukushauri usitoe mimba ni hizi zifuatazo-
1. watu wengi walishapatwa na tatizo kama lako, waliacha watoto wakazaliwa na wanaishi mpaka leo. tena ww una nafuu mm nina uncle wangu mke wake alipata mimba ya pili wakati mtoto wa kwanza alikuwa na miezi 9, hawakutoa bali lihudhuria clinic zote tena ilikuwa kijijiini na alijifungua salama na huyo mtoto na mwenzake wamemaliza sekondari,ukiwaona unaweza kudhani ni mapacha. hivyo, usitoe mwache mke wako azae chini ya usimamizi wa daktari
2. kutoa mimba ni kosa la jinai ndio maana mara nyingi hufanyika vifichoni na huleta madhara makubwa kuliko hata kuacha mtoto azaliwe chini ya uangalizi wa daktari
3. kutoa mimba kunaleta madhara makubwa ya kisaikolojia/kiakili ya kudumu kwa mwanamke na nafsi yake haitapata amani kamwe na ukimshawishi atakuja kukulaumu baadae na kusababisha ndoa yako kukosa amani
4. katika mambo ya kidini kutoa mimba ni sawa na kuua ambayo huleta laana kwa familia nzima na kwa kila aliyeshiriki.Inajumuisha kukosa furaha moyoni, kuzaa watoto wasio watii, kuwa tasa, kukosa amani katika doa,kuwa na hukumu ya moyoni yaani hilo tukio hutalisahau kabisa litakuhukumu daima
Jiulize hivi mama yako angetoa mimba yako je ww ungekuwepo leo?
msikilize Mungu na mwombe Mungu atakupa kuzaa huyo mtoto bila tatizo,
umenielew?