Mimba inatutesa!

MAKULUGA

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2011
Posts
7,828
Reaction score
10,527
Mke wangu anaujauzito wa mwezi mmoja huu ni ujauzito wake wa3 !Ila cha kushangaza unampeleka puta kwa kutapika mfululizo hadi amekonda kwa kutokula chakula cha kutosha kwa wiki mbili sasa ,hivi hakuna dawa za kupunguza hali hii kwa kuwa imekuwa mbaya kuliko kawaida tuliyoizoea ! Kabla hatujaenda kwa daktari najua humu ntapata nuzoefu wa kutosha!
 


  • Kujisikia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)

    Nusu ya wanawake wote wajawazito hupatwa na tatizo la kujisikia kichefu chefu na kutapika; ni mojawapo ya dalili kuu za ujauzito.


    Husababishwa na kuongezeka kwa hormone mwilini, mara nyingi huanza katika wiki ya sita ya ujauzito na huweza kutokea muda wowote wa siku.


    Madaktari wengine huwa wanaamini ya kuwa ni dalili nzuri kwani humaanisha ya kuwa placenta inafanya kazi vizuri.


    Kwa wanawake wengine tatizo hili huisha katika wiki ya kumi na mbili ya ujauzito. Lakini kwa wengine huweza kuendelea kwa kipindi kizima cha ujauzito.


    Mara nyingi ni kitu cha kawaida ambacho kinakuja na kuondoka lakini pale ambapo mama anatapika kupita kiasi mpaka anashindwa kubakisha chakula au maji mwilini basi anahitaji kumuona daktari.





    Vitu vya kufanya kusaidia au kupunguza tatizo hili:

    1. Kula milo mingi midogo mara kwa mara badala ya kula milo mikuu mitatu kwa siku. Hii itasaidia kwasababu wakati mwingine tatizo hili linasababishwa na kutokuwa na sukari ya kutosha kwenye damu(low blood pressure). Sukari hii ndio chanzo cha nguvu mwilini. Ukila mara kwa mara chakula kitapokelewa mwilini na kutengenezwa sukari na mwili kuwa na nguvu ya kutosha.
    2. Kunywa vinywaji nusu saa kabla au baada ya chakula. Usinywe vinywaji na kula chakula kwa wakati mmoja.
    3. Kula mkate wa kukausha(toast au crackers) au matunda yaliyokaushwa dakika 15 kabla ya kumka asubuhi.
    4. Kunwya maji mara kwa mara ili kuzuia mwili kuishiwa na maji (dehydradtion). Jaribu kunywa litre 2.5 kwa siku ikiwa pamoja na maji, chai au juice natural zisizo na sukari ya kuongeza.
    5. Jitahidi usile au kupita sehemu zenye harufu ya chakula zinazozidisha tatizo hili.
    6. Pumzika vya kutosha na pata usingizi wa mchana.
    7. Usikae sehemu zenye joto jaribu kukaa ndani kwenye feni au ac au nje sehemu zenye upepo. Kwasababu joto huzidisha tatizo hili. Pia usiende sehemu zenye watu wengi.
    8. Ndimu, tangawizi zinasaidia, pia unaweza kunywa maji ya ndimu au kula tunda la tikiti maji (watermelon) kupunguza kichefu chefu.
    9. Kula viazi vya kukausha na chumvi.
    10. Fanya mazoezi.
    11. Usilale baada ya mlo
    12. Usiache kula
    13. Usile au kupika vyakula vyenye pili pili (spicy) au mafuta mengi.
    14. Usinywe kahawa au vinywaji vikali
    15. Kula vyakula vya protein kabla ya kwenda kulala usiku
    16. Fungua madirisha au Tembea nje ili kupata upepo na oxygen ya kutosha.
    17. Weka kijiko kimoja cha maji ya Apple Cider Vinegar kwenye 8 ounces ya maji ya uvuguvugu kisha kunywa asubuhi kabla ya kuamka.


    [TABLE="class: cms_table, align: center"]
    [TR]
    [TD] [/TD]
    [/TR]
    [TR]
    [TD]Maji ya Apple Cider Vinegar[/TD]
    [/TR]
    [/TABLE]


    18. Kunywa chai za Rasberry leaf, Spear mint/ pepper mint, Anise seed, Fennel seed kabla ya kuamka asubuhi.
    [TABLE="class: cms_table, align: center"]
    [TR]
    [TD] [/TD]
    [/TR]
    [TR]
    [TD]chai ya raspberry leaf[/TD]
    [/TR]
    [/TABLE]

    [TABLE="class: cms_table, align: center"]
    [TR]
    [TD] [/TD]
    [/TR]
    [TR]
    [TD]chai ya anise seed[/TD]
    [/TR]
    [/TABLE]



    [TABLE="class: cms_table, align: center"]
    [TR]
    [TD] [/TD]
    [/TR]
    [TR]
    [TD]chai ya fennel seed[/TD]
    [/TR]
    [/TABLE]





    Kunywa chai ya Tangawizi itakuzuia Kichefu chefu na Kutapika.



    Umwone daktari kama:


    Unatapika kupita kiasi mpaka unashindwa kubakisha chakula au maji tumboni au kama kutapika kunaambatana na homa au maumivu. chanzo.
  • Topic: Kujisikia kichefuchefu na kutapika wakati wa ujauzito (Morning Sickness)





 

Attachments

  • Tangawizi ni tiba ya kichefu chefu.jpg
    52.1 KB · Views: 372
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…