- Source #1
- View Source #1
Kisukari cha mimba (Gestational diabetes - GD au GDM) ni aina ya kisukari kinachotokea wakati wa ujauzito, ambapo kiwango cha sukari kwenye damu hupanda kupita kiasi (hyperglycemia).
Hali hii hutokea pale homoni zinazozalishwa na kondo la nyuma (placenta) zinapoathiri uwezo wa mwili kutumia au kutengeneza insulini ipasavyo. Insulini ni homoni inayosaidia mwili kudhibiti kiwango sahihi cha sukari (glucose) kwenye damu.
Dalili za kisukari cha mimba
Dkt. Rugemeleza anaeleza kuwa dalili hizi hufanana sana na dalili za kawaida za ujauzito, ni rahisi kuzichanganya; hivyo uchunguzi wa kitabibu ni muhimu sana ili kugundua tatizo mapema.
Dalili Zinazoonekana: Mama mjamzito anaweza kuwa na kiu kinachopita kiasi na kukojoa mara kwa mara.
Athari za kisukari cha mimba
Dkt. Isaac Rugemalila, Daktari Bingwa Mbobezi wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila anabainisha athari zifuatazoi.
Athari kwa Mama: Sukari iliyozidi inaweza kuharibu mishipa ya damu na viungo muhimu kama figo na ini. Vilevile, hupunguza ufanisi wa mfuko wa uzazi (kushuka kwa uchungu), jambo ambalo linaweza kusababisha mama ashindwe kujifungua kwa njia ya kawaida na kulazimika kufanyiwa upasuaji.
Athari kwa Mtoto: Mtoto hupokea sukari nyingi sana kutoka kwa mama, na anapojaribu kuitunza mwilini mwake, husababisha akue na kuwa na uzito uliopitiliza. Tatizo hili pia linaweza kusababisha mtoto kufia tumboni kabla ya kufikia ukomavu stahiki.
Nani yupo kwenye hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu?
Mwanamke yeyote anaweza kupata kisukari cha mimba wakati wa ujauzito. Hata hivyo, kuna baadhi ya mambo yanayoweza kuongeza uwezekano wa kupata hali hii, ikiwa ni pamoja na:

- Kuwa na ugonjwa wa moyo.
- Kuwa na shinikizo la juu la damu.
- Kuwa na uzito mkubwa kupita kiasi (obesity) au uzito uliopitiliza kabla ya ujauzito.
- Kuwahi kupata kisukari cha mimba katika ujauzito uliopita.
- Kuwa na historia ya kisukari cha aina ya pili (Type 2 diabetes) katika familia.
- Kuwa na ugonjwa wa ovari wenye vifuko vingi (Polycystic Ovary Syndrome - PCOS).
- Kupata ujauzito katika umri mkubwa wa uzazi.
- Kuwa na prediabetes (hali ambapo kiwango cha sukari kwenye damu huwa juu kuliko kawaida lakini bado hakijafikia kiwango cha kisukari).