Mimba isiyotarajiwa

Mimi sijapanic wala kumpanikisha binti, nimemsapoti toka mimba hadi kujifungua.
Ishu ya kutumia kinga mara nyingi hua mwanzoni ila mazoea yakizidi unajikuta tu unaenda kavu. I declare the defeat
 

Sasa mama hizo hasira nyingi za nini? Binti alkua anajua kua mi nko na mahusiano yangu.
Tafsiri utakavyotafsiri, kama unaona ni hasira or whatever, its OK. Ila umeleta mada katika jukwaa huru na hayo ni maoni yangu. Na hata ungekuwa mwanangu msimamo wangu ungebaki hivyo.
Usiandike kwa kuwa unataka furahisha watu, ukweli unaujua wewe na Mungu wako kama huyo binti ulimwambiaje mnapoanza mahusiano. Kama nae alikubali kudate nawe akijua huna future nae wote mtakuwa na shida.
Kingine , kama umeweza msaliti huyo uliye na malengo nawe kabla hata hujamuoa, ukioa itakuwaje.

Sikuchukii kwa kuwa hata kukujua sikujui, ila nakupa ushauri, kaa chini tafakari na badili mwenendo. Wewe ni mzazi, na utaendelea kuzaa ukijaaliwa, wanao wakikua utaelewa maumivu na changamoto za malezi.

Msimamo wangu utabaki palepale kuwa umevuruga future ya huyo binti na mtoto aliyemzaa. Take it o live it
 
😅😅 karoti haikutoshi, ongeza na bamia hapo. Iko hivi... nilikutana nae mwanzoni mwa mwaka jana ( mwez wa 3) kajifungua last week ( wiki la mwisho la disemba) au ushajisahau leo ni 2024 bro.
Hapo nimekuelewa sasa sio ile kauli "baada ya mwezi then last week akajifungua"
 
🙆🙆🙆
 
Ila we nae unamatatizo kwa hiyo huyo mwenye uko nae serious ndio unamuona wa maana sana.
Umeharibu maisha ya binti wa watu alafu sa hii ety ng'ong'ong'og'o.
Ww muoe huyo binti huyo mwingine muache ataolewa na kina mshamba_hachekwi
 
Mama bhana, sasa nimfurahishe mtu hanijui na simjui? Ndio maana hili ni jukwaa huru napost kwa watu tofaut ambao hawanijui wala siwajui, niwadanganye ili iweje sasa? Nahitaji solid ideas kwa watu wasonijua ili wawe very free kufunguka. There was no point ya mi kudanganya kwa watu siwajui ili kupata ushauri,,, it make no sense to me.

Anyway pole kwa yaliyokukuta kama mzazi. Binafsi najua nlipozingua that's why nkaomba ushauri ili nisiendelee kuharibu. Sasa we umekuja na hoja za kuvuruga future ya mama na mtoto.. sasa sijui huo ndo ushauri wako?
Sorry! Em naomba nieleweshe
 
Kabisa, halafu wanatudanganya sana🚮
 
Pole Sana, nazijua nyakati unazopitia.
 
Anyway pole kwa yaliyokukuta kama mzazi. Binafsi najua nlipozingua that's why nkaomba ushauri ili nisiendelee kuharibu. Sasa we umekuja na hoja za kuvuruga future ya mama na mtoto.. sasa sijui huo ndo ushauri wako?
Sorry! Em naomba nieleweshe
Mpendwa, hakuna lililowai nikuta na siombei yanikute. Nimelelewa katika maadili, hata mtoto wangu wa kwanza nimezaa nikiwa katika ndoa halali nikiwa na miaka 28. Nina binti wà miaka 7, nitapambana na ninamuombea kwa Mungu yasimkute. Sikukuandikia kukukwaza ila nilikutaka ukae chini utafakari maana nakuona ili suala umechukulia kirahisi bila kuangalia madhara. Sikukushauri kwa kuwa unao msimamo kuwa una mchumba tayari, so nikatoa ushaur kwa wote ili tujifunze kupitia kesi yako.
Kwa kuwa umetaka maoni yangu nitakupa ushauri.

1. Usimuoe huyo bint kama humpendi. Usijilazimishe wala usilazimishwe. Ni heri akabaki na maumivu haya, kuliko kuingia kwenye ndoa ambapo hapendwi. Hamtakaa kwa amani na madhara yake ni makubwa zaidi

2.muoe huyo binti. Jilazimishe kwa kujifunza kumpenda. Wapo waliochaguliwa wenza na wazazi, sio kuwa walipendana, ila walijifunza kupendana, kujaliana na kuheshimiana. Na wamedumu.

3. Ukishindwa kumuoa, mwezeshe, ili asiwe tegemezi kwako wala wazazi. Wazazi wake washamaliza kazi ya kulea, so mzigo wa kulea ubaki kwenu. Hudumia mwanao na mpende, na kamwe usimfiche kwa ndugu wala mkeo ajae.

Huo ndio ushauri wangu. Na msimamo wangu utabaki uleule.

*tunajifunza kupitia makosa ya wengine
 
Muoe huyo Binti, anza naye maisha na Mungu atawajalieni familia yenye furaha na upendo. Kinyume chake karma is really
 
Kuna life style unayopanga kuishi,afu Kuna life style unayopangiwa. Maamuzi unayo wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…