Mimba tatu zimeharibika

Kayenga jr

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2016
Posts
443
Reaction score
349
Ndugu wana JF doctor,

Nimekuja kuomba ushauri nipo ndani ya ndoa mwaka wa nne nimekuwa nahangaikia kutafuta mtoto bila mafanikio.

Mke wangu amewahi kushika mimba kama Mara tatu zote zinatoka ndani ya mwezi mmoja tu nimehangaika nilianzia hospital ya kumpeleka wife vipimo vyote vilikuwa vipo sawa kama hormone, ultra sound, na vinginevyo kasoro kipimo kinachoitwa HSG.

NikampelakaRecency Hospital inaonesha mrija mmoja umeziba kwa ushauri wa doctor akasema mmoja anaweza kupata mtoto sasa tatizo ni muda mrefu sasa hata ile kushika tu imekuwa tatizo.

Nimeanza tena haraka upya vipimo vipimo vyote havina mabadiriko kwani hata nimepima nipo vizuri isipokuwa wife alifanya kipimo flan pale TMJ ikaonyesha ana virus flan vinaitwa Rubbela akapatiwa dawa ila tatizo bado ujauzito haupatikani nimeshauriwa akafanye tena HSG hapo ndio pananichanganya maana mzunguko wake Upo sawa na haubadiriki badiriki sema akiwa period ndio unaweza kumuonea huruma tumbo kuuma.

Nimeshawahi kujaribu kwa Dr Mwaka ila sikuona mafanikio zaidi ya kuwa napewa hadithi ambazo hazina uhakika.

 
Ndugu wana JF Doctor nimekuja kuomba ushauri nipo ndani ya ndoa mwaka wa nne nimekuwa nahangaikia kutafuta mtoto bila mafanikio.

Mke wangu amewahi kushika mimba kama Mara tatu zote zinatoka ndani ya mwezi mmoja tu nimehangaika nilianzia hospital ya kumpeleka wife vipimo vyote vilikuwa vipo sawa kama hormone, ultra sound, na vinginevyo kasoro kipimo kinachoitwa HSG.

Nikampelaka Recency Hospital inaonesha mrija mmoja umeziba kwa ushauri wa doctor akasema mmoja anaweza kupata mtoto sasa tatizo ni muda mrefu sasa hata ile kushuka tu imekuwa tatizo.

Nimeanza tena haraka upya vipimo vipimo vyote havina mabadiriko kwani hata nimepima nipo vizuri isipokuwa wife alifanya kipimo flan pale TMJ ikaonyesha ana virus flan vinaitwa Rubbela akapatiwa dawa ila tatizo bado ujauzito haupatikani.

Nimeshauriwa akafanye tena HSG hapo ndio pananichanganya maana mzunguko wake Upo sawa na haubadiriki badiriki sema akiwa period ndio unaweza kumuonea huruma tumbo kuuma.

Nimeshawahi kujaribu kwa Dr Mwaka ila sikuona mafanikio zaidi ya kuwa napewa hadithi ambazo hazina uhakika.
 
Nimejikuta naimba wimbo huu "Tazama, wewe ni Bwana; Mungu wa wote wenye mwili. Je kuna neno gumu lolote? Usilo liweza? Je kuna neno, kuna neno, kuna neeno? Usiloo liweza? Je kuna neno gumu lolote? Usiloo liweza"
 
Kama Mungu alifanya kwa watu wa zamani ,akafanya kwa vzazi vya sasa na leo pia yupo tayar kufanya kwako kama utamtegemea.Wala usijiingize katk imani potofu we piga got ongea na Mungu wako.Mungu anasubir upeleke hoja zako mbele zake naye atafanya
 
Kama Mungu alifanya kwa watu wa zamani ,akafanya kwa vzazi vya sasa na leo pia yupo tayar kufanya kwako kama utamtegemea.Wala usijiingize katk imani potofu we piga got ongea na Mungu wako.Mungu anasubir upeleke hoja zako mbele zake naye atafanya
Asante kaka
 
Miaka minne sio mingi hadi ukate tamaa, kinacho kucost hadi sasa ni pressure uliyonao inayotoka kwa marafiki, ndugu pamoja na majirani wanaokuzunguka. Tuliza akili yako mkuu weka imani yako kwa Mwenyezi Mungu halafu anza kutafuta solution ukiwa na amani moyoni mwako, usipanic hilo ni jaribu lako nawe huna budi kulishinda
 
Poa pamoja
 
Wee acha tu yaan
Ila kwa7bu ulishapima ukaonekana upo safi na doc kasema shemeji anaweza akafanikiwa kupata ujauzito nadhani ni kumwachia tu Mungu atatenda kwa wakati wake,wengine wanakaaga miaka kumi muhim nikuheshimiana na kufarijiana ndani ya nyumba,pia utulivu uwepo mengine yatajiset yenyewe,Abraham alipata mtoto akiwa na 80yrs kaka Mungu ataleta neema hakukupa mke then asikupe mtoto.
 
piga moyo konde ipo siku kama sio leo hta kesho pengine mwenyezi amewaandalia kitu kinzuri hapo baadaye
mtegemee yeye siku zotee
najua fulaha ya ndoa ni mtoto ila mpende na mvumilie mkeo
mwenyezi mungu akuoongozeee
 
Pole sana, kwanza ondoa hofu, I miaka 4 sio mingi, hasa kama utaishi maisha yako wewe na mkeo bila kuruhusu ndugu/marafiki kuwaingilia.

Nime pitia katika hali kama yako, na japo ina tofauti kidogo, namshukuru Mwenyezi Mungu sikuwapa ndugu/marafiki nafasi la sivyo ningekuwa na hali mbaya.

Mkewangu kwanza alichopewa kushika ujauzito, mpaka mwaka wa kwanza wa ndoa ukaisha. Ndani ya miezi 3 tu ndugu/marafiki washaanza kuulizia kama tayari.

Kuja kushika mimba, zinatoka mara 2, mara ya 3 ikatungwa nje ya kizazi na tukachelewa kugundua mpaka ikapatikana na akaanza kuboresha ndani, akifanyiwa upasuaji.

Tuli hangaika sehemu mbalimbali mpaka kwa Dr Mwaka na kwa maspecialist ila kikubwa sote tulikuwa hatuna hofu sana wala shauku kwasababu tulikuwa tuna imani kuwa mtoto anatoka kwa Mwenyezi Mungu.

Baada ya mahangaiko Mwenyezi Mungu akujaalia kushika tena na sasa unaelekea mwezi wa tatu Alhamdulilahi hakuna tatizo lolote kubwa mpaka sasa.


Kubwa, kwanza tambua mtoto ni baraka kutoka kwa Allah subhanahu wataala, hivyo msiwape presha sana tambueni wakati ukifika kama karanga mpate mtoto mtapata tu.

Pili kuwa karibu sana na mkeo na hata kama una hamu sana na mtoto jitahidi usi muonyeshe na untie moyo, tambua kuwa wana wake ndio wanao umia zaidi katika hali kama hiyo hivyo wewe ndio msaada wake mkubwa.

Kubwa na la mwisho usijidanganye kutoka nje ya ndoa kwenda kutafuta mtoto, unaharibu kabisa dira ya maisha yenu, zinaa ni deni na malipo yake yana tisha kabisa

Endelea kukazana na kutafuta tiba na kumtegemea Mwenyezi Mungu, yeye ndie ajuaye ghaibu.

Kuna bibi mmoja chanika mkewangu aliwahi kutibiwa huko, ana dawa nzuri na za gharama nafuu, kama hauja wahi kujaribu huko nta kutafutia mawasiliano yake.
 
Tatizo lako limeshagundulika huna haja ya kuhangaika. Mini Mke Wangu anatatizo kama la Mke wako mrija mmoja umeziba. Alikuwa na tatizo la kuugua kwa masaa yasiyopungua kumi mfululizo anapokuwa mwezini Ila tatizo la maumivu liliisha baada ya kufanyiwa operation ya kuzibua mirija kwa kukata na kuunga tena Ingawa operation hiyo haikufanikiwa. Nyama kubwa ilitolewa wakati wa operation ndio iliyokuwa ikimuumiza. Suala la kushika mimba mwanamke akiwa na mrija mmoja inawezekana Ila ni mtihani sana. Suluhisho la tatizo lako ni kufanya invetro fertilization hii ni kutunga mimba nje na kupandikiza ndani ya mfuko wa uzazi. Mimi Nimepata mtoto baada ya miaka kumi na tano ya ndoa kwa njia nilivyokuambia. Njia hii ni Gharama na Mimi nilifanyia nje ya nchi. Ila kwa uwezo wa Mungu Mke Wangu Alipata ujauzito kwa njia ya kawaida na kupata mtoto baada ya miaka 18 ya ndoa. Kwahiyo usihangaike hiyo ndio hali halisi ni mtihani unaohitaji subira ya Mungu kama huna uwezo wa kufanya IVF kama nilivyofanya Mimi. Ila siku hizi unaweza jaribu hata hapo Kenya kwa Gharama nafuu kati ya Dola elfu sita hadi nane Ila hii nayo ni kujaribu tu unaweza pata au kukosa Mimi nilijaribu mara tano mfululuzo hadi kuja kufanikiwa. Mungu yupo na anatenda mtegemee Yeye.
 
Nakushukuru sana kwa ushauri kaka mungu akubarikia ningeomba kama utapata mawasiano ya huyo bibi sio mbaya nikajaribu njia zote za kienyeji na hospital
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…