Mimba tatu zimeharibika

Mimba tatu zimeharibika

Pole sana...lakini waweza tumia virutubisho vya fur seal oil na phytoestrogen vitakusaidia kushika mimba kwa haraka sana na kuimarisha mfumo wako wa uzazi...wasiliana nasi kwa namba 0653299934
Vinapatakana wapi kwa faida ya wengine
 
Duuh! Pole sana!

Asante ndugu. Nawashauri wanaume wenzangu kuwa na busara sana unapokabiria na changamoto kama hii. Wanawake msione wa kipiga kelele lakini ni viumbe delicate sana wanaohitaji msaada wetu sana hasa kipindi kama hiki. Wanaume tunatakiwa kuwa na huruma na wake zetu, kutosikiliza pressure za kifamilia na kuwa tayari wakati wote kujitoa muhanga kuwasaidia hawa kina mama kadri ya uwezo wetu ambao Mungu ametupatia. Tusiwanyanyase wala kuwanyanyapaa katika kipindi hiki kigumu na Tumtegemee Mungu sana yeye naweza kila kitu.
 
Asante sana kwa ushauri tatizo ni hizo gharama nachosubiria kwa sasa ni kufanya hicho kipimo cha HSG tena ili kuona je huo mrija bado umeziba? Na kitu ambacho sikielewi mwanamke mirija ikiziba mzunguko wake (kwa maana ya period) anapata kama kawaida?

Mimi sio daktari lakini kuziba kwa mirija hakuathiri mzunguko wa mwanamke kwakuwa mke wangu hajawahi poteza mzunguko wake hata mara moja. Nadhani hormones imbalance ndizo zinazosababisha mzunguko kubadilika. Pole sana nakutakia kila la kheri na ukitaka kunishirikisha mimi kikwelikweli katika aina yeyote ya msaada niambie kwakuwa nimeuishi uchungu ulionao kwa miaka kumi tano na siku kumi na tano. Allah atakuafu mtegemee yeye. Kila la kheri katika kila la kheri mnalokusudia kilifanya na Allah awafanyie wepesi juu ya hayo mnayokusudia kufanya na amapatie mama huyo ustaamilivu na wepesi juu ya shida zake. Amen.
 
Asante sana kaka kwa msaada wako na ushauri Mungu atuongoze katika mtihani huu
 
Ndugu wana JF doctor nimekuja kuomba ushauri nipo ndani ya ndoa mwaka wa nne nimekuwa nahangaikia kutafuta mtoto bila mafanikio.

Mke wangu amewahi kushika mimba kama Mara tatu zote zinatoka ndani ya mwezi mmoja tu nimehangaika nilianzia hospital ya kumpeleka wife vipimo vyote vilikuwa vipo sawa kama hormone, ultra sound, na vinginevyo kasoro kipimo kinachoitwa HSG.

NikampelakaRecency Hospital inaonesha mrija mmoja umeziba kwa ushauri wa doctor akasema mmoja anaweza kupata mtoto sasa tatizo ni muda mrefu sasa hata ile kushuka tu imekuwa tatizo.

Nimeanza tena haraka upya vipimo vipimo vyote havina mabadiriko kwani hata nimepima nipo vizuri isipokuwa wife alifanya kipimo flan pale TMJ ikaonyesha ana virus flan vinaitwa Rubbela akapatiwa dawa ila tatizo bado ujauzito haupatikani nimeshauriwa akafanye tena HSG hapo ndio pananichanganya maana mzunguko wake Upo sawa na haubadiriki badiriki sema akiwa period ndio unaweza kumuonea huruma tumbo kuuma.

Nimeshawahi kujaribu kwa Dr Mwaka ila sikuona mafanikio zaidi ya kuwa napewa hadithi ambazo hazina uhakika.
Isije ikawa hiyo wanaita endometriosis
 
Dogo chalaza hiyo 'k' mpaka ibadirike rangi iwe nyekundu, mimba itaingia tu sasa maana hakuna namna!!
Wewe umenichekesha kweli. Umenikumbusha kijana mmoja sijui ni teja akawa anamwambia mwenzie," Huyo mtoto bonge hivyo kumzaa kazi sio ndogo, lazima upige mabao mawili"
 
Mwambieh mkeo aandike hitaji lake na ambatanishe na sadaka aiombee baada ya hapo apelekee kanisa lolotee au msikitin if Muslims na awe na imani Mungu atatenda jambo juu yenu...
Nawaombeeh furaha na amani..
 
Mpeleke kanisa la ukombozi kwa nabii malisa Ana upako wa kusaidia watoto kuzaliwa.pia kuna majini mahaba nayo yanafanya mimba kuharibika...chukua hatua hizo ni hila za shetan
 
Kaa na huyo mwanamke mkubaliane utafute mtoto nje huku mkiendelea kutafuta wa kwenu
 
Relax miaka minne michache sana Kaseja Juma tangu kaoa zaidi ya miaka 9 mke wake Nasra kajifungua juzi
 
Napata mashaka huenda mkeo Kabla hujamuoa alikuwa bingwa wa kuabot Mimba za mwezi miezi miwili mitatu matokeo yake uzazi umejenga tendency kwa hiyo akishika Mimba ikishafika umri ule aliokuwa anatoa toa na yenyewe inatoka. kuhusu kutoshika Mimba Tena huenda kuna uvimbe kwenye kizazi ndiyo maana Akiwa hezi Anaumwa Sana. waone wataalam wapime kwanza kizazi alafu tulia Miaka miwili ndipo utafute Tena Mimba
 
Akipata mimba Tena MPE DAWA inaitwa duphastone itakaa nilikuwa na tatizo hilo but now nns mtoto
 
Poleni sana kwa changamoto zinazowakabili. Ni vyema mngefanya vipimo vya kutosha wote wawili ikiwemo hormones. Je alishawahi kupima hormones muhimu kipindi cha ujauzito?

Mie sio dr ila uzoefu unaonesha kuwa kama progesterone level zipo chini sana kwa mjamzito mimba kutoka ni rahisi...hii inaandaa uterus kwa ujauzito..inasaidia lining na hata kusapoti fetus mpaka pale placenta itapo-takeover.

Je, kipindi mkeo mjamzito lishawahi pima hizo hormones? ikiwemo estrogen na progrestone?

Kuwa na mrija mmoja mke anaweza pata ujauzito ingawa kuna changamoto.

Kama mna uwezo mnaweza fanya ivf...(but still itafanikiwa zaidi pale mtakapojua chanzo cha mimba zenu kutoka) hivyo uchunguzi wa kina kwa mkeo unahitajika.

Ila kubwa kuliko lote ni kumtanguliza Mungu, yeye atafanya njia
 
poleni sana kwa changamoto zinazowakabili. Ni vyema mngefanya vipimo vya kutosha wote wawili ikiwemo hormones. Je alishawahi kupima hormones muhimu kipindi cha ujauzito?
mie sio dr ila uzoefu unaonesha kuwa kama progesterone level zipo chini sana kwa mjamzito mimba kutoka ni rahisi...hii inaandaa uterus kwa ujauzito..inasaidia lining na hata kusapoti fetus mpaka pale placenta itapo-takeover. Je kipindi mkeo mjamzito lishawahi pima hizo hormones? ikiwemo estrogen na progrestone?

kuwa na mrija mmoja mke anaweza pata ujauzito ingawa kuna changamoto.
kama mna uwezo mnaweza fanya ivf...(but still itafanikiwa zaidi pale mtakapojua chanzo cha mimba zenu kutoka) hivyo uchunguzi wa kina kwa mkeo unahitajika.

ila kubwa kuliko lote ni kumtanguliza Mungu, yeye atafanya njia
Proved mirija yote imeziba kwa mujibu wa kipimo cha HSG nilichoambiwa ni operation ndio kinachofata hakuna njia nyingine hapa Mawazo tu yananisakama
 
Ndugu wana JF doctor nimekuja kuomba ushauri nipo ndani ya ndoa mwaka wa nne nimekuwa nahangaikia kutafuta mtoto bila mafanikio.

Mke wangu amewahi kushika mimba kama Mara tatu zote zinatoka ndani ya mwezi mmoja tu nimehangaika nilianzia hospital ya kumpeleka wife vipimo vyote vilikuwa vipo sawa kama hormone, ultra sound, na vinginevyo kasoro kipimo kinachoitwa HSG.

NikampelakaRecency Hospital inaonesha mrija mmoja umeziba kwa ushauri wa doctor akasema mmoja anaweza kupata mtoto sasa tatizo ni muda mrefu sasa hata ile kushuka tu imekuwa tatizo.

Nimeanza tena haraka upya vipimo vipimo vyote havina mabadiriko kwani hata nimepima nipo vizuri isipokuwa wife alifanya kipimo flan pale TMJ ikaonyesha ana virus flan vinaitwa Rubbela akapatiwa dawa ila tatizo bado ujauzito haupatikani nimeshauriwa akafanye tena HSG hapo ndio pananichanganya maana mzunguko wake Upo sawa na haubadiriki badiriki sema akiwa period ndio unaweza kumuonea huruma tumbo kuuma.

Nimeshawahi kujaribu kwa Dr Mwaka ila sikuona mafanikio zaidi ya kuwa napewa hadithi ambazo hazina uhakika.
nilipatwa na shida hiyo ila baada ya kumuona Dr. Kapona mambo yameenda fresh saivi nina vidume viwili,alikuwa hapo tumaini hospital,akaenda THI saivi ana hospitali yake Chanika buyuni jaribu kupita pita huko mkuu
 
Proved mirija yote imeziba kwa mujibu wa kipimo cha HSG nilichoambiwa ni operation ndio kinachofata hakuna njia nyingine hapa Mawazo tu yananisakama

kama operation itasaidia fanyeni. ingawa sioni uhusiano wa mirija kuziba na mimba kutoka. all in all ikishindikana mkafanye IVF, tena kama mna uwezo nendeni nje ya nchi angalau wenzetu hufanya uchunguzi wa kina kabla ya tiba (madr wa bongo msinipopoe mawe ndio ukweli wenyewe) yaani i wish mchunguzwe vizuri wewe na mkeo.
 
Back
Top Bottom