Ndugu wana JF doctor nimekuja kuomba ushauri nipo ndani ya ndoa mwaka wa nne nimekuwa nahangaikia kutafuta mtoto bila mafanikio.
Mke wangu amewahi kushika mimba kama Mara tatu zote zinatoka ndani ya mwezi mmoja tu nimehangaika nilianzia hospital ya kumpeleka wife vipimo vyote vilikuwa vipo sawa kama hormone, ultra sound, na vinginevyo kasoro kipimo kinachoitwa HSG.
NikampelakaRecency Hospital inaonesha mrija mmoja umeziba kwa ushauri wa doctor akasema mmoja anaweza kupata mtoto sasa tatizo ni muda mrefu sasa hata ile kushuka tu imekuwa tatizo.
Nimeanza tena haraka upya vipimo vipimo vyote havina mabadiriko kwani hata nimepima nipo vizuri isipokuwa wife alifanya kipimo flan pale TMJ ikaonyesha ana virus flan vinaitwa Rubbela akapatiwa dawa ila tatizo bado ujauzito haupatikani nimeshauriwa akafanye tena HSG hapo ndio pananichanganya maana mzunguko wake Upo sawa na haubadiriki badiriki sema akiwa period ndio unaweza kumuonea huruma tumbo kuuma.
Nimeshawahi kujaribu kwa Dr Mwaka ila sikuona mafanikio zaidi ya kuwa napewa hadithi ambazo hazina uhakika.