Mimba ya miezi 8 na siku 17 je, Kuna uwezekano kujifungua na mtoto akawa hai?


1: Si kila maumivu yanayowapata wajawazito kipindi cha kuelekea ukingoni mwa ujauzito ni uchungu (labor pain). Unahitaji kumwona mtaalamu wa afya kujua kama huo ni uchungu halisi.

Uchungu halisi huusisha(maumivu kuongezeka ukali kila muda unavyopita, muda wa maumivu kutokea(maumivu-maumivu/interval ) hupungua kadri muda unavyokwenda na muda wa ukaaji wa maumivu(duration) huongezeka.

2: Kuzaa mtoto wiki ya 36-37 bado inacheza pata potea ya kupata mtoto ambaye hajakomaa vyema.
Watoto hao hukabiliwa na tatizo kwenye: upumuaji(RDS), kujitengenezea joto lake la mwili, upotevu wa maji mwilini.

3: Ni vyema unapopata mtoto wa wiki 37 au chini ya hapo, kuwe na wataalamu wa kutosha kumhudumia mtoto njiti na mazingira toshelevu.

4: Ukomavu mzuri ni kuanzia wiki ya 38-40 na siku 3.

Mtoto atazaliwa kabla ya muda wake kwa sababu kiasili zisizozuilika kiasili au kwa sababu ya kuokoa uhai wa mama.
 
Peleka Mkeo Hospitali acha kuhangaika na maswali ambayo hata ukijibiwa hautaelewa.Kama ana dalili za uchungu mpeleke hospitali Daktari ataamua kama wakati tayari au BADO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…