Kulizungumzia suala ya kutoa mimba kunahitaji tafakuri ya kina na wakati mwingine kuvaa viatu vya wahusika wa suala hilo.
Hebu fikiria binti ni tegemezi kwa asilimia 100 na familia yake ipo ktk kundi la mafukara, binti amegeuzwa kuwa kiburudisho/mfariji wa ngono na mchovu mwenzake, inatokea mimba anaikana kwa sababu hana uwezo/hataki majukumu Huyo binti afanyeje? hapa ni bora aitoe ili aendelee na maisha yake.
Pia kwa sehemu kubwa mahusiano ya cku hizi ni ya kuburudishana zaidi ya kujenga familia, vijana(me) wengi bado wapo wapo sana kuhusu suala la kuanza kununua pampas,n.k, na wengine hawataki kabisa kuzaa na watu ambao hawatakuja kuishi nao kwa hiyo mimba ikizalishwa aidha binti akubali itolewe au iwe yake, sasa ni juu ya binti ana uwezo wa kuitunza, familia je-itamuunga mkono au ndo mwanzo wa mateso?