Mwanamke hata atembee na wanaume wangap na akapata mimba atajua tu kwamba hii mimba n ya fulan
Na pind tu mimba inapoingia tuseme sekunde mwanamke hutambua. Cjui uwezo aliowapa mungu
Sasa naomba kujuzwa ni dalil zp hua anazi sense mwanmke pind 2mimba inapoingia au ni mabadliko gan hua anayapta ndan ya huo mda mfupi
Nawsilisha wadau
Mpaka sasa hakuna kipimo ambacho kinaonyesha moja kwa moja kama ujauzito (Mimba) umeingia mpaka kusubiri kwa mda wa siku 7 mpaka 10 baada ya mbegu za kiume kukutana na yai (Urutubishaji) .
Hizi zifuatao ni dalili10 za ujauzito.
1. Kukosa mzunguko wa hedhi (Peridod)
Hii ndio dalili kubwa ambayo watu wengi huijua wakati mwingine mtu anaweza akakosa period ndani ya mda unaotakiwa kutokana na sababu za kiafya, mazingira au hata mawazo akaanza kufkiria kuusu ujauzito sababu kukosa mzunguko ni dalili mojawapo ya ujauzito. Ingawa wakati mwingine mtu anaweza akawa mjamzito lakini akaendelea kupata period kipindi cha mwanzo.
2. Homa za asubuhi
Mara nyingi hizo homa za asubuhi huwa kipindi cha miezi mitatu ya kwanza (first trimester) ingawa pia baadhi huendelea hadi second trimester (miezi mitatu ya pili). Ila wakati mwingine hizi homa za asubuhi huja kutokana na sababu za ulaji.
3. Mabadiliko ya matiti na chuchu
Mwanzo pia unaweza ukaona mabadiliko ya matiti ambayo ni kama:-
- Matiti kuuma au kuvimba (Au vyote kuuma na kuvimba).
- Chuchu kubadilika rangi.
- Chuchu husisimka zinapoguswa.
- Unaweza ukaona mishipa ya damu kwenye maziwa.
- Sehemu ya chuchu kuongezeka ukubwa.
4. Ute ute kuongezeza ukeni
Kuwepo kwa ute mwingi mwingi kwenye uke. Baadhi ya wanawake hupata kidogo ila baadhi hupata mwingi kiasi cha kuwabugudhi.
6. Uchovu
Pindi unapopata ujauzito mfumo wa umeng`enyaji chakula huongezeka ili kukidhi mtoto na mama na hapo ndipo uchovu hutokea. Kama utajisikia kulala inabidi ulale bila kujizuia.
7. Kukojoa mara kwa mara
Wiki moja baada ya kutunga mimba mjamzito huenda haja ndogo mara kwa mara lakini hutoa mkojo kidogo sana. Hali hii hutokea sababu kiini huanza kutoa kemikali ya hCG.
8. Kuchukia au kupenda baadhi ya harufu
Wakati mwingine mjamzto hupenda hata harufu mbaya. Na baadhi ya harufu ambazo ulizipenda kabla hapa utaanza kuzichukia.
9. Kutokea kwa Pimpozi na chunusi
Hutokea kipindi cha mwanzo cha ujauzito. Pindi zikitokea usizitoe wala kuzitumbua sababu zitaacha madoa kwenye uso wako.
10. Kubadilika kwa rangi ya uke
Kutokana na kuongezeka kwa damu sehemu za fupanyonga basi husababisha uke kuwa na rangi ya uzambarau kuliko kawaida.
Source:
google