Mimea ina akili?

Mimea ina akili?

Mimea Huhisi Maumivu Katika Quran​

Januari 21, 2023 Miujiza ya Quran

Mimea Huhisi Maumivu Katika Quran​

?
Quran 17:44
Zinamtakasa mbingu saba na ardhi na vilivyomo ndani yake. Na hakuna chochote isipokuwa kinamtukuza Mwenyezi Mungu kwa sifa zake, lakini nyinyi hamufahamu jinsi wanavyotakasika. Hakika Yeye ni Mpole na Msamehevu.

📖 Quran 22:18
Je, huoni kwamba vinamsujudia Mwenyezi Mungu vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini na jua na mwezi na nyota na milima na miti na viumbe vinavyotembea na watu wengi ? Lakini juu ya wengi adhabu imehalalishwa. Na ambaye Mwenyezi Mungu amemdhalilisha, hana wa kumstahi. Hakika Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.

  • Imethibitishwa kisayansi kwamba mimea hutoa machozi au maji ili kujilinda kutokana na athari mbaya za bakteria na kuvu. Madhumuni ya maji haya ni kupigana na vimelea vya magonjwa, kudhibiti na kudumisha viwango vya unyevu vyema kwenye majani, na kwa usafiri wa virutubisho kwenye mmea.
  1. Rejea : Je, Mimea Hulia?
  2. Mimea Marejeleo Ina Hisia Pia

Taarifa za ziada

Quran inachukuliwa kuwa kitabu cha miujiza kutokana na uwezo wake unaotambulika wa kutoa mwongozo, hekima, na kutabiri matukio yajayo. Ufasaha wake na uzuri wake wa kifasihi pia huchukuliwa kuwa miujiza na wengi. Zaidi ya hayo, Waislamu wanaamini kwamba Quran ina habari za kisayansi ambazo hazikujulikana wakati ilipoteremshwa na kwamba huo ni ushahidi wa asili yake ya kimungu. Hii ni pamoja na habari juu ya embryology, astronomy, na nyanja zingine za sayansi, Waislamu wanaamini kwamba uhifadhi wa Quran na ukweli kwamba imebaki bila kubadilika kwa zaidi ya miaka 1400 pia ni muujiza.
🙏🙏🙏
 
Ngoja mmea wako ukue uvuke na fensi uende kwa jirani ako ndio utajua kua mmea. Una akili au akili una mmea.
Bado hujasema.
 
Ngoja mmea wako ukue uvuke na fensi uende kwa jirani ako ndio utajua kua mmea. Una akili au akili una mmea.
Bado hujasema.
Yaani niugharamie mimi halafu matunda uyapeleke kwa jirani? Sitauruhusu!!!
 
Mimea ina nguvu ndani yake,ipo mimea usinyaa ikiguswa,ipo mimea hula wadudu akitua tu inajifunga analiwa,ipo mimea ina nguvu za kuzuia nguvu za wachawi na majini wasiweze kuingia eneo nyumba au shamba.
Ipo mimea inayovutia nyoka na isiyovutia pia.
Ipo mimea ndani ya nyumba kama hakuna amani haikui inasainyaa,ipo mimea uleta bahati,nk
 
Mimea ina nguvu ndani yake,ipo mimea usinyaa ikiguswa,ipo mimea hula wadudu akitua tu inajifunga analiwa,ipo mimea ina nguvu za kuzuia nguvu za wachawi na majini wasiweze kuingia eneo nyumba au shamba.
Ipo mimea inayovutia nyoka na isiyovutia pia.
Ipo mimea ndani ya nyumba kama hakuna amani haikui inasainyaa,ipo mimea uleta bahati,nk
Mkuu, mimea inakula "wanyama?" Ina mfumo ya kuweza kumeng'enya wadudu?
 
Huku machakani tunatumia mimea kugundua planted mines (Mabomu) katika eneo husika.
Bioengineered.
Nahisi wewe ni msoja!

Huwa mnafanyeje mkuu? Tueleze japo kidogo tu. Tutoe tongo tongo, huenda na sisi tukapata idea ya kuitumia kufanyia gunduzi zenye manufaa.
 
Je mumea hauhisi maumivu unapokatwa?[emoji16]
Mimea ina kitu kinachosense stimuli mbali mbali.
Mfano Geotropisim - Mmea huelekea upande tofauti na nguvu ya uvutano wa Dunia na Jua.
Phototropisim - Mmea hukua kuelekea uelekeo wenye mwanga wa jua.
Mmea umeumbwa na uwezo wa ku sense mimea iliyo jirani kwa kutumia vitu kama vile kivuli kutambua kusa kuna mmea jirani hivyo kuufuata.
 
Ipande mpwa mix colors zote nyumbani utapaona kama paradise....sema migumu kidogo kuota ukiwa na dhambi flaniflani haioti ukipanda😁
Mimea ina utambuzi wa dhambi? Dhambi gani labda?

Ni wapi ninakoweza kupata mbegu yake jijini Mwanza?
 
Nadhani unauliza kwa nini mimea inayokua kwa kulanda ina uwezo wa kukua kufuata sehemu ya kujiegemesha. Kwa kawaida, mimea inayokua kwa kulanda ina uwezo wa kukua kufuata sehemu ya kujiegemesha kwa sababu ya phototropism. Phototropism ni uwezo wa mimea kukua kuelekea chanzo cha mwanga. Hata hivyo, mimea inaweza kukua kufuata sehemu ya kujiegemesha kwa sababu ya gravitropism. Gravitropism ni uwezo wa mimea kukua kuelekea chini kwa sababu ya mvuto wa ardhi. Kwa hiyo, mimea inayokua kwa kulanda inaweza kukua kufuata sehemu ya kujiegemesha kwa sababu ya gravitropism
 
Back
Top Bottom