Tangu nifunge ndoa na mke wangu, yeye amekuwa akisisitiza kuwa na house girl, kila anayekuja anakuwa na vituko vya jabu, na wa mwisho ambaye tumemfukuza jana alikuwa eti ana majini tukisali na kulitaja jina la yesu anasumbuka, eti akawa anaomba tusisali na tukienda church tumuache. Sasa mimi nimemueleza wife tutafute mtu wa kuja kwa kutwa ila yeye eti anasisitiza mpaka mtu wa kuishi naye, unajua namshangaa, na ndiyo utamaduni wa wanawake woote sijui, mambo eti housgirl, housegirl, wanawake mtakoma lini?
maelezo yako mkuu ninaona hayajakamilika , umuhimu wa house girl unategemea na familia yako ilivyo. kama mkeo anafanya kazi basi ni muhimu kuwa na msaidizi, kama hafanyi kazi-yaani anashinda hme tu na hakuna watoto wadogo sana zaidi ya mmoja unaweza kusemna hahitajiki.
house girl nyumbani anasaidia
1. kazi za ndani
2. back up ya shughuli nyingine wakati wa dharula ndani ya family- kwamfano waweza mtuma mbali na nyumbani , mkoa mwingine kukuwakilisha ktk jambo lolote
3. ni walinzi pia, kwani unauhakika nyumbani kuna mtu- hili hasa kama wote hamshindi nyumbani na ni watu wa kusafiri
sasa housegirl wa kuja na kuondoka jioni faida zake ni kuwa
hahitaji kuwa mtu wa utamaduni au imani inayofanana na familia yako, kwakuwa anakuwa kazini muda mfupi tu.
hasara yake , ni kuwa
1. kwa kuja na kuondoka manake ni lazima umlipe mshahara wa mtu unaotosha kulipa nyumba na bills za umeme, maji nk
2. kwakuwa anatakiwa kujitegemea kila jambo huko anakokaa, wengi hushawishika kuwa wadokozi hapo ndani kwako au hata kuleta wezi wakubwa- kumbuka anahitaji kujilipia gharama za maisha.
ushauri wangu ni huu;
1. kama unaweza kumlipa kati ya 150,000-200,000 waweza chukua wa kuja na kurudi jioni, otherwise utajiingiza kwenye hasara kubwa
2. kwa kutumia sala na maombi utapata house girl mzuri, omba Mungu, uwe mvumilivu utampata siku moja. usimlaumu tu mkeo
kwaheri