SoC02 Mimi Figo, sikilizeni kilio changu naumia

SoC02 Mimi Figo, sikilizeni kilio changu naumia

Stories of Change - 2022 Competition

Clark cian

Senior Member
Joined
Jul 3, 2021
Posts
154
Reaction score
146
''Kilio cha figo kimekuwa ni cha kimya kimya kinachotoa madhara makubwa kadri mda na wakati unavyosonga,mataabiko na misukosuko ambayo figo inapitia,mtaani kwetu imezua gumzo na watu wameanza kutunga nyimbo mbalimbali kusihi watu juu ya utunzaji wa Figo zao kwa ajili ya kuokoa maisha yao"

Nawasalimu kwa jina la 'jamii forum stories of change',ni matumai mu wazina na afya,basi pale jua lichomozapo ndipo harakati za maisha huanza tena !!afya ni kitu cha muhimu sana kwenye maisha yetu bila kuwa na afya bora basi maisha lazima yawe duni

''Naitwa Erasmy Lashau naishi Moshi maeneo ya Majengo, mpaka kufikia leo imepita miezi sita tangu jirani yetu ambaye alikuwa baba wa familia(jina limehifadhiwa) afariki kutokana na kufeli kwa Figo kufanyana kazi ''renal failure'' katika HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, sio siri yeye ndo alikuwa tegemezi sana kwenye familia yake ya watoto wanne! wa kwanza akiwa na miaka 25 na wa mwisho miaka 4; kwakuwa alikuwa ni mzazi pekee nyumbani baada ya mama yao mzazi kufariki baada tu ya kujifungua mtoto wao wa mwisho {kiukweli ni jambo la kusikitisha sana} .

Wazazi wameacha watoto wadogo ambao bado walikuwa wanahitaji matunzo na malezi kutoka kwa wazazi wao,lakini yote kwa yote mungu anasaidia gurudumu la maisha linaendelea ijapokuwa ni kwa shida sana kwasababu kulelewa na ndugu siku zote hawawezi leta upendo wadhati kama wazazi wanavyolea watoto wao wa kuwazaa. Na hiyo yote ni kutokana na mtindo wa maisha aliyokuwa akiishi baba huyo kwenye uhai wake unywaji pombe kali kwake zilikuwa ni sifa, maji kunywa akijisikia na sasa amecha watoto wanne ambao hawana baba wala mama, maisha yao ya manyanyaso kila siku, vilio usiku kucha haviishi mpaka kuna wakati tunasema ni makelele kumbe ni sauti za kinyonge za watu wanaoonewa daah! inaniuma sana na sitaki kabisa kijana aliyehai kuiga mitindo ya maisha inayoleta madhara kwenye viungo vyetu muhimu vya mwili.

Sasa baada ya figo kulia sana bila kusikika na baba mzazi huyo; ikaacha kufanya kazi kutokanan na manyanyaso yaliyosababishwa na pombe kali alizokuwa akitumia mzazi huyo basi mzazi akafariki na kuacha taifa nyuma likimtegemea .

Sasa nimeamua kusimama leo kwenye jukwaa hili kwa mara ya kwanza mimi kama kijana wa miaka 22 kutoa makala muhimu kuwasihi WATANZANIA tuwe na mtazamo chanya juu ya afya za figo zetu ili kunusuru kizazi chetu katika karne hii ya teknolojia ya halii ya juu'' kutokana na simulizi hili nimeandaa makala sahihi kuhusu afya za figo zetu na jinsi ya kuzuia changamoto hizo ili kuongeza siku za kuishi.
source thestrip.ru

UTANGULIZI
Katika makala hii nimewaandalia vitu vichache ambavyo vitaweza kuweka figo zetu katika afya sahihi endapo tukifuata na kuishi kwenye maisha yetu ya kila siku
  • MAANA HALISI YA FIGO
  • KAZI SAHIHI ZA FIGO
  • VYANZO VYA HITILAFU NA MAGONJWA YANAYOSHAMBULIA MWILI KUTOKANA NA FIGO KUSHINDWA KUFANYA KAZI
  • UTAJUAJE KAMA NI MMOJA WA WENYE TATIZO KWENYE FIGO
  • UTAJUAJE KAMA UNAKASORO KWENYE UTENDAJI KAZI WA FIGO
  • JINSI YA KUEPUKANA NA MAGONJWA YA FIGO

Nini maana ya figo?
Figo ni kiungo katika mwili cha kutatanisha ambacho kazi yake kuu ni kuchuja damu na hivyo kuondoa taka mwili zote kupitia njia ya mkojo mfano huondoa chumvi chumvi zilizozidi mwilini ambazo hupelekea madhara kwenye mifumo ya damu pamoja na neva pia. Kwa hiyo ukiachana na ini ambalo hufanya kazi nyingi kuliko viungo vyote mwilini ambapo hufuatiwa na fiigo ambapo ni kiungo muhimu sana kwenye miili yetu hivyo tunaaswa kutunza afya za figo zetu kwa kuzingatia kanuni za afya juu ya figo zetu.

source gettyimage

Figo hushughulika na nini kwenye mwili?
Tukiachana na kazi kuu ya figo kwenye uchujaji wa damu pia kutokana na tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanasayansi juu ya figo imebainika kuwa figo ni kiungo cha chakustaajabisha kutokana na kufanya kazi zaidi ya moja kazi hizo hufanywa mara tu baada ya uchujaji wa damu kama;

Uwekaji sawa wa kiwango cha maji kwenye mwili
Uwekaji sawa wa kiwango cha asidi na alkali katika mwili
Utengenezaji wa vitamini D ambayo ni muhimu sana kwenye ukuaji wa mifupa imara na yenye afya
Huongoza utengenezaji wa seli nyekundu za damu kutokana kuzalisha homoni au kichochezi kiitwacho erythropietin

Angalizo: Endapo tukileta utani au mzaha kwa figo zetu hupelekea madhara makubwa kwenye mifumo yetu yote katika mwii kama methali isemavyo 'mzaa mzaa hutumbua usaa ' basi ni vizuri kulijadili swala hili kiundani ili kuweza kuondoa matatizo yatokanayo na kudhoofika kwa figo

Ni vipi vyanzo vya hitilafu na magonjwa yanayoikumba figo?
Kwenye karne hii ya 21 watu wengi hasa vijana wamekuwa hawajali afya zao na kula kila vyakula bila kujali matokeo yake hivyo kupelekea madhara katika mfumo wa utoaji taka mwili ikiwemo figo na mifumo mingine kwenye mwili hivyo kupelekea kifo hivyo kupunguza nguvu kazi kwenye ngazi ya familia hadi taifa .Kwahiyo zifuatazo ni baadhi ya vyanzo vya hitilafu katika figo

Unywaji wa pombe kali kupitiliza ambapo huenda kuzuia utoaji sahihi wtvichochezi 'hormone' zinazoenda kusaidia kwenye uwekaji sawa wa maji na elekrolaiti "electrolyte" mwilini mfano kalsiam ,pia utumiaji wa juisi za kikemikali mfano Energy drink ni chanzo kikubwa cha figo kushindwa kufanya kazi

Mwili kukosa maji ya kutosha ,ambapo moja kwa moja husababisha uwezekano mkubwa wa kupata ugonjwa wa majiwe ya figo 'kidney stones' ambapo itahitajika upasuaji ili kuyaondoa

Utumiaji wa madawa ya kutuliza maumivu,mfano ibuprofen na naproxen moja kwa moja hushusha ufanisi wa figo katika ufanyaji wa kazi zake

Ulaji wa kiasi kikubwa cha protini ;ambapo pia hupelekea msukumo wa juu wa damu kwenye figo


Utajuaje pia kama unaugonjwa au hitilafu katika figo?
  1. Shinikizo la damu
  2. Kuvimba miguu, mikono pamoja na uso
  3. kuwa mdhaifu mwili kuchoka na kupungua uzito
  4. kukosa hamu ya chakula na kujiskia kichefuchefu na kutapika
  5. Kukojoa damu ,pia mkojo kuwa na sukari au protini

Nitafanyeje ili kutunza afya ya figo yangu?
- Ulaji wa mlo kamili na kuepuka visababishi vya hitilafu kwenye figo mfano pombe kali,protini nyingi,kahawa nyingi na unywaji holela wa dawa za kutuliza maumivu
source.https://www.shutterstock.com

Mwisho kabisa
Tushirikiane kuzuia magonjwa ya Figo ili kujenga taiga imara na familia bora kwa maendeleo
unaweza fuatilia makala zaidi kupitia Kidney Education Foundation
 
Upvote 7
Asante kwa mada nzuri inayoelimisha.

Energy drink ni chanzo kikubwa cha figo kushindwa kufanya kazi
Kama vinywaji vya energy vina madhara kiasi hiki, basi serikali ilaaniwe kuamua kuua kabisa kizazi kijacho kwa kuruhusu utengenezaji na uuzwaji holela wa hii sumu kwa vijana wetu.
mzaa mzaa hutumbua usaa ' b
Hapa ; mzaa = mzaha
Usaa = usaha.
 
Asante kwa mada nzuri inayoelimisha...
Exactly boss hapa serikali imeacha kuangalia namna gani ya kuokoa vijana na kujikita zaidi kwenye masuala ya tozo na kujenga nchi huku wakibomoa kwa upande mwingine
 
Back
Top Bottom