DocJayGroup
JF-Expert Member
- Jan 17, 2020
- 1,654
- 3,346
Introduction: Mimi sio mwanasiasa, mimi ni mjasiriamali. Shughuli zangu ni Pamoja na media, tourism, lodging, na transport services. Pia nafanya shughuli kati ya nchi ya Tanzania na USA. Ujasiriamali una faida sana, lakini pia una changamoto hasa ukiwa unasimamisha biashara mpya.
Napenda kufuatilia watu waliofanya mambo makubwa maishani, na mmojawapo ni Tiger Woods. Kama haumjui, mfuatilie Google, lakini yeye ni mtu mweusi aliyetesa sana wzungu kwa miaka mingi katika mchezo wa golf. Msemo mmoja anaoutumia sana TW, unasema “Winning takes care of everything.” Manake kwa Kiswahili ni kwamba “ushindi katika mchezo/ maisha ni kila kitu.”
Kwenda USA - Dharau Kisha Heshima: Mimi nakumbuka nikiwa nashughulikia mambo yangu ya kwenda USA. Nilikuwa kijana mdogo sana, nimechaguliwa kwenda Kibaha High School kusomea PCB kutokea Ilboru Secondary. Lakini baada ya kusoma tu muhula mmoja Form V, dili/ fursa ya kwenda USA ikajitokeza. Hio ilikuwa ndoto yangu hasa mtoto kutoka familia maskini sana niliamini kwenda abroad kutanitoa kimaisha. Jambo ambalo lilikuja kuwa kweli. Basi niliacha shule Form V ili kushughulikia fursa hio.
Nilitukanwa sana na watu wengi kwamba mimi ni mjinga na nimeachaje shule nzuri nazurura tu? Tena baba sina, na mama ni maskini ninafikiriaje nitaenda USA. Tiketi nitatoa wapi nk. Matusi mengi sana nilipewa hasa majirani walikuwa wananibeza hata nasikia kabisa. Ila watu hawakujua mipango yangu, ila siku napaa majuu, heshima ikaanza. Nikawa nakuja Tz kila mwaka ku-show off (nilikuwa mtoto na mjinga enzi hizo), na heshima ikazidi kweli. Kila mtu akawa ananiita mzee. Mademu wote wananitaka, na masela wote wanataka kuwa kwa crew yangu.
Maisha Leo - Ushindi Unaendelea: Off course nilikuja kutuliza akili baadaye na kufanya mambo ya maendeleo na ya maana kabisa, na heshima ikaja kuzidi hadi leo. Dhumuni la kusema haya ni kuonyesha kwamba pesa ukiwa nayo, kwa wengi ni kila kitu na wanakuona mshindi sana kimaisha. Unapata heshima kubwa, unapata watu wengi wanataka kukufanyia kazi kwa hio una chagua tu top yao, wafanyakazi wanajitahidi sana kufanya kazi kukupendeza ambayo ina faida kwa biashara. Kwa sababu hizo napambana na pia namwomba Mungu ili aendelee kunipa ushindi, manake sitaki kushindwa kimaisha, kibiashara, au kifedha.
About Magufuli: Magufuli ni mtu anayepitia challenges nyingi kama rais. Mimi sio CCM wala CHADEMA, mimi ni independent voter. Kiukweli lakini, sipendi kuona CCM imekosa challenge miaka yote hii, kwa hivyo nategemea siku moja watatoka madarakani ili at least mwingine ajaribu naye.
Lakini mtu upende usipende, hadi sasa JPM ni mshindi na mwanaume kwelikweli. Na si kwamba hakosi changamoto, lakini utakuta kwa changamoto nyingi anazopitia mwisho wa siku anaibuka mshindi. Ndege zake zimekamatwa sijui mara ngapi, ila kila mara wanaziachilia. Mpaka wa Zambia wengi tulisoma Habari zimeandikwa umefungwa, sasa jana usiku ma-lorries yameachiliwa na kuendelea na safari kiulaini kabisa.
Mwaka jana shilingi iliporomoka sana wengi tukafikiria Tanzania itakuwa Zimbabwe, ila walifanya yao, shilingi ikasimama tena vs other currencies. Sasa hivi wengi wamesema hajafanya lockdown, ila WHO nao wamesema COVID19 inawezekana watu ikabidi wajifunze kuishi nao. Mimi kwa Marekani naishi Los Angeles USA, kuna gazeti linasema “We shut down the economy to make progress against COVID-19 — and then made no progress”. Manake walifanya lockdown ili kupata ushingi dhidi ya COVID19, lakini hali bado ni mbaya. Manake JPM hajafunga kitu, na mwisho wa siku anaweza kuonekana alikuwa sawa kutokana na mambo kama haya.
Conclusion: Bado Tanzania ina changamoto nyingi. Mfano ajira kwa vijana, walimu na wengineo ni tete, mishahara ya wafanyakazi wa UMMA haijaongezewa kwa muda, na vitu vinapanda bei kama sukari nk. Lakini Magufuli kweli sio kwamba hapati changamoto, anazipata sana, lakini kwa asilimia kubwa anapambana na anasimama.
Tumuombee afanye maamuzi busara, na tuombee hayo matatizo mengine yapate ufumbuzi manake ya ajira nk. Kwa hivyo jambo nimejifunza kwa JPM mimi kama mjasiriamali ni kwamba mwisho wa siku, ushindi ni muhimu sana. Mambo yanaweza yumba, lakini ni muhimu kupambana hadi kupata ushindi, sababu hata waliokupinga, huwa wananyamaza tu kimya kabisa kama ukiibuka mshindi.