DocJayGroup
JF-Expert Member
- Jan 17, 2020
- 1,654
- 3,346
- Thread starter
- #21
La muhimu ni kufanya jambo ambalo ni legal ili kutimiza malengo. Legal manake pasipo kuvunja sheria. Moral au kufuata maadili ni jambo lingine. Manake jambo linaweza kuwa legal lakini likawa sio moral. Mtu ukawa haujavunja sheria lakini jambo umetenda halina maadili.Kwa hiyo mkuu,,
unatufundisha tuwe wanafiki inapobidi na kujipendeza kupitiliza ili kutimiza malengo eti?
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuwa mnafiki na kujipendekeza kupitiliza hakujakaa kimaadili sana lakini ni legal. Kwake yeye Bashite alimjua Jiwe na kutambua ili aendelee kuwa mtoto wake mpendwa ni lazima afanye kila kitu baba anafanya. Watu kama Nape Nauye walifanya vingine na mwisho wa siku bado wakaenda ikulu kupiga magoti. Mimi baada ya Mwigulu kuachishwa uwaziri nilimshauri jambo, na akafanya hivyo hivyo. Na sasa amerudi uwaziri. Sijisifii, lakini kuna mambo katika maisha nayafahamu sababu nimetokea sifuri hadi nilipo leo nimefanikiwa namshukuru Mungu.
Cha kujifunza hapo ni strategy tu. Kujipendekeza au kuwa mnafiki sio kuzuri. Somo hapo ni kwamba mtu ili kufanikiwa, ni lazima uchague strategy ambayo itakufanikisha wewe binafsi na malengo yako.
Na ndio nilimtaja Jack Ma, kamwe hakosoi Chinese govt sababu anajua matokeo yatakuwaje. Au wadada wanaofanya porn, wao malengo yao yametimia japo wanachofanya sio maadili.
Pia tujifunze kuwa mwisho wa siku, sio lazima kufurahisha watu. Tujiangalie sisi wenyewe na malengo yetu. Manake hata kama jambo sio moral kwa watu, kama ni legal na ndio lengo letu la maisha, tusiangalie wengine watatusema vipi.