Kuna neno fulani la kizungu linaitwa "Enlightment Period" Ila sitawezeza kulifanyia tafsiri sisi kabisa kwenye mjadara huu. Ila kwa kifupi ni kipindi ambacho yaliyo mema na mazuri ambayo yanasifiwa na kufurahisha na kuonekana yalipata kufanyika kwenye nyakati hizo.
Wanajanangwani kwa sasa wamemaliza kipindi chao hiko, ambapo itawapasa wachukue tena miaka 3 ijayo kujitengenezea enlightment period nyingine kwenye tasnia ya soka.
Kusua sua kwake msimu huu kunadhihirishsa wazi kuwa nyakati zao sasa zimekwisha, na kipindi cha mwingine. Hivyo basi bila kusema mengi ningependa kuwatakia Azam FC ushindi mnono hapo Jumamosi watapokutana na Yanga SC. KUna uwezekano ikawa isiwe dhahiri kuwa ni enlightment period ya azam fc lakini siku zote waswahili wanasema "nyota njema huonekana asubuhi", na hatma haiumbwi na kisicho dhaniwa.
Licha ya ukimya wao naona kabisa Azam FC wanafaa kuwa mabingwa wa ligi kuu msimu 2017/18, hivyo basi hata kulingana na shaka yangu izaliwayo na muenendo wa Yanga SC napenda kuweka wazi kuwa nawatakia ushindi mnono walamba koni ifikapo jumamosi.
Kabla sinatamatisha andiko,
Niseme kuwa kila klabu kubwa ulimwenguni yenye kupitia kwenye "enlightment period" ni lazima ipumzike kwa muda mfupi ili kupisha mabadiliko ya nyakati kabla haijarudi kwenye kipindi chake.
Kwa mfano :-
Timu yenye mafanikio makubwa nchini Uhispania "Real Madrid" iko kwenye kipindi hiko hiko cha mpito.
Timu yenye mafanikio makubwa uingereza "Manchester Unite" iko kwenye kipindi hiko hiko cha mpito.
vile vile
Timu yenye mafanikio makubwa Tanzania "Yanga SC" iko kwenye kipindi hiko hiko cha mpito.
ANGALIZO:-
Kipindi hiko cha mpito huwa hakidimu kwa zaidi ya miaka 3, ukiona timu iko kwenye kipindi cha mpito kwa zaidi ya miaka 3, Tambua kuwa haikuwahi kuwa kwenye "Enlightment Period". Kigezo pekee cha timu kuwa kwenye Enlightment period kuanzia miaka 10 na kuendelea.
Nawasilisha,
Demigod-