Hili neno Mabingwa wa kihistoria, huwa nasikia wanalitumia sana baadhi ya watangazaji wa radio, sasa linaanza kuenea kwa wasikilizaji wasiotafakari maneno.
Historia ni profile, kutoka ulipoanzia hadi ulipo hivi sasa, kwahiyo tukija kwenye mpira wa miguu, mfano: Timu A, inasifa ya kuchukua vikombe vingi, itakua imetengeneza profile yake kwa kuchukua makombe mengi.
Timu B, ina vikombe vichache pia itakua imetengeneza profile yake.
Timu C, yenyewe haina kombe ni kufungwa michezo yote, nayo pia itakuwa imetengeneza profile yake kwa sifa zake.
Kwahiyo historia ni profile yako uliyoitengeneza, na kwamwe sio haina maana kufanya vizuri.
Timu ya Mtibwa wamewahi kuchukua ubingwa wa bara nayo ni historia.
Huwa sielewi ninaposikia Wanahabari, wanaaminiwa wakitumia Kiswahili kisicho na maana, Katika Lugha hiyo Adhimu.
cc, SIBONIKE.