Mimi Masudi Kipanya na safari yetu ya miaka 100

Mwnangu umetoa dozi ya kutosha kwa mzee mwenzangu ambaye utumwa wa kidini ulimharibu kiasi cha kutojua asubuhi ni lini na usiku ni lini. Nadhani ametoa uzi huu akidhani naye ni maarufu kiasi cha kuhangaisha watu wakijadili mkutano wake na Masudi. Nadhani angeeleza hoja au cha mno cha mkutano huu kwa jamii, ingependeza.
 
Mzee Mohamed, hongera sana kwa kutujuza na kutupatia mafunzo mengi kupitia makala zako! Barikiwa sana! Hakika wewe ni Manju Uliyebobea katika Mawanda Mapana ya Historia, Uandishi Vitabu, Habari na Makala Mbalimbali! [emoji120]
Obe...
Ahsante sana.
 
Father...
Nimefanya kipindi na Masudi kitakachorushwa mwezi mzima na Clouds Plus king'amuzi ni DSTv.

Sikueleza maudhui kwa makusudi.

Hili la kuwa mimi ni maarufu au la kwa hakika si mimi wa kusema hilo.

Ila kwa ufupi nitakufahamisha kuwa nimezaliwa Gerezani ambayo ni sehemu ya mji wa Dar es Salaam.

Nimeishi hapa maisha yangu yote na naamini wanamji wengi wa rika langu si kuwa wananifamu mimi bali hata wazee wangu.

 

Attachments

  • VID-20210427-WA0049.mp4
    60.6 MB
Watu wanaomtetea huyu Mzee hawamfahamu vizuri ndio mana
 
heko
 
BABU YANGU SALUM ''NDEGE MWEMA'' ABDALLAH NA KIGOMA CHA DAKU

Naiaga Ramadhani kwa kutabaruku na babu yangu Salum Abdallah (Allah amrehemu yeye na wazee wetu wote waliotangulia mbele ya haki) na kigoma chake cha daku na nyimbo iliyokuwa haipigwi ila pale wapigaji watakapofika nyumbani kwetu.

Inaelekea nyimbo hii alitungiwa yeye makhsusi.

Ramadhani ya mwaka wa 1965 nikiwa na umri wa miaka 13 ikanikuta Tabora nilipokwenda kumtembelea babu alipotoka jela.

Maghrib ikikaribia uwanja mbele ya nyumba yetu unafagiliwa na majamvi yanatandikwa adhana ikipigwa futari zinaanza kutolewa na kufunikwa na makawa makubwa.

Baada ya kushuka msikitini watu wanakaa kufuturu.

Watu wengi walikuwa wanakuja kufuturu pale nyumbani.

Sikumbuki katika miaka ile kuona watu wakila chapati, sambusa, na mapochopocho mengine kama futari katika miaka ile.

Siku zile futari ni mihogo, maharage, kunde, ndizi mzuzu na ndizi mbivu na uji wa pilipili manga, chai ilikuwa si sana labda kama sikui ile kuna kuja wageni kufuturu.

Tabora ndiko nilikojifunza kula mihogo iliyoungwa kwa karanga badala ya nazi vyakula vyote hivi vilikuwa vinatoka shambani kwetu.

Unywaji wa chai katika kufuturu ulikuwa nadra.

Wala hapakuwa na unywaji wa juisi.
Hivi vitu vimekuja miaka hii ya hivi karibuni.

Sielewi kwa nini ilikuwa vile ni hali za watu au ndivyo ilivyotakiwa iwe?

Sasa nakuja kwa babu.

Baada ya sala ya tarweh watu hukaa wakazungumza kuvuta muda wa daku na pale nyumbani kwa babu ndipo ilikuwa barza kubwa ya mtaa watu wakikutana hapo.

Niliambiwa miaka ile ya kupigania uhuru miaka ya 1950 hapo ndipo taarifa zote za Nyerere zilipokuwa zikipatikana na watu kutiana moyo kuwa Muingereza siku zake zinahesabika uhuru unanukia.

Baada ya uhuru ghafla ndiyo balaa likamkumba babu yangu kwa kukamatwa na kuwekwa kuzuizini kwa tuhuma kuwa alikuwa katika njama za kupindua serikali ya Nyerere babu na viongozi wengine wa vyama vya wafanyakazi akihusishwa na maasi yale.

Barza ile ya babu ilipooza alipokuwa kifungoni kwani marafiki zake wengi walikata mguu kufika pale na hata alipotoka Jela ya Uyui ile ingia toka kama ya zamani haikuwapo.

Hakuna aliyetaka kunasibishwa na mtu ''haini.''

Lakini juu ya haya kuna watu hawakumtupa mkono babu walikuja kila siku ya mwezi wa Ramadhani kumuimbia nyimbo ambayo ilikuwa haimbiwi yeyeyote mji mzima isipokuwa yeye babu yangu.

Nyimbo hii ilikuwa inaitwa ‘’Ndege Mwema.’’

Mashairi yake yalikuwa yakimsifia babu kwa ubinadamu na ukarimu wake.

Tabora kigoma cha daku ni tofauti na vigoma vya dafu kwengineko ambako yanapigwa matari peke yake.

Tabora kigoma cha daku kina ngoma nyingi kigoma cha daku kinapigwa kwa staili ya mchanganyika wa ngoma za Kimanyema na Waswezi na nyimbo zake zina ‘’melody,’’ za kuvutia.

Kigoma cha daku wakishamuona huko wanakotoka babu kakaa nje sasa watakuwa wanakuja nyumba baada ya nyuma wanasimama na kupiga kwa dakika moja mbili wanazima wanaendelea hadi wanakaribia nyumba yetu.

Kabla ya kufika mapigo yanabadilika na lile goma kubwa utalisikia sasa likirindima na sauti za waimbaji utazisikia zikiimba kwa masikitiko.

Wanafika mbele ya babu hapo ndipo utazisikia ala zinazungumza.

Babu kakaa kajiinamia kama vile ngoma zile zinampeleka mbali sana.

Baada ya muda atanyanyuka atawafata huku anafungua pochi yake kuwatunza.

Watazima muziki kisha watapiga mwimbo mwingine kwa mdundo wa kuondoka na kwa mdundo huo watamuaga babu.

Babu hapo na yeye ataondoka kuingia ndani.

Maisha yake yote babu yangu aliishi na tuhuma ya kutaka kupindua serikali lau kama ilikua ni uongo.

Alipofariki dunia mwaka wa 1974 TANU ilifika katika mazishi yake na walisoma risala nzuri sana ya kumsifia kwa mchango wake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa mwanachama wa TANU na akiwa kiongozi wa TRAU wakamsifia kwa ukarimu wakasema kuwa mkono wake siku zote ulikuwa wazi akitoa kwa ajili ya nchi yake.

Huyu ndiye babu yangu na kigoma cha daku na mwimbo wake, ‘’Ndege Mwema.’’

PICHA: Salum Abdallah (mshale) kuliani kwake ni Kassanga Tumbo.
 
Huyu mzee anajua historia ya kariakoo tu sio tanzania nzima
 
Huyu mzee anajua historia ya kariakoo tu sio tanzania nzima
Mdukuzi,
Nimesoma historia kwa kiwango cha chuo kikuu.
Nimeandika vitabu 10.

Nimeshiriki katika kuandika Dictionary of African Biography (DAB) mradi wa Harvard na Oxford University Press, New York nikiwa pia mshauri.

Hii ni kamusi ya volumes 6 na imeshachapwa 2011.

Nimeshiriki katika mradi wa kuandika historia ya nchi za Afrika Mashariki kwa shule za msingi.
Kitabu changu kimechapwa mwaka wa 2007.

Sijui historia ya Kariakoo bali naijua historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na hii ni historia ya wazee wangu wao ndiyo walioasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) 1933 na kuunda TANU 1954.

Kariakoo ndiyo yalikuwa makazi ya hawa babu zangu na mimi nimezaliwa hapo.
 
Umesoma historia kwenye chuo kikuu kipi?

Tafadhali naomba utujuze na utuambie umemaliza mwaka gani huko Mohamed Said
 
Hongera
 
Tatizo moja wewe Masudi Kupanga ni mnafiki namba moja Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…