0909Hekima
JF-Expert Member
- Feb 23, 2013
- 226
- 65
Habari wana jamvi wenzangu, leo nimeona nije na jambo la kushare nanyi kwani nimeona wajasilia mali wenzangu wakiongelea biashara na ujuzi wao waliokuwa nao na kushare nanyi, nawapongeza wote kwa mawazo yao yenye msaada mkubwa kwetu sote na pia nitachukua nafasi hii kujaribu kutoa elimu kwa uchache ya ujasilia mali na itakuwa ni yenye mwendelezo kama mtaona ni yenye kuwafaa.
MJASILIA MALI AMEUMBWA KWA MAMBO MAKUU MATATU KAMA YAFUATAYO:
1. Knowledge and skills; kwa maana ya kuwa awe na ujuzi na kile kitu anachotaka kufanya, hii itamuwezesha mjasilia mali kuwa katika nafasi nzuri ya kukifanya kitu kwa ufanisi na mazingatio ya hali ya juu sana, kama unataka kufuga hakikisha unapata elimu kwanza juu ya ufugaji na juu ya mfugo unaotaka kuufuga, hili litakupelekea kuwa katika nafasi nzuri juu ya biashara, the same kwa mkulima au mfanya biashara yoyote.
2. Ability; hii ni ule uwezo wa mtu kufanya jambo fulani, determination!!! Fanya juu chini Biashara unayotaka kufanya iwe ndani ya UWEZO WAKO!! MTAJI, ENEO, nk. vyote viwe ndani ya uwezo wako, epuka jambo lolote ambalo utahisi hautaweza kulimudu kwani kila mbuzi hula kwa urefu wa kamba yake, anza padogo na mtaji utakapoongezeka basi nawe jipanue wigo wako, epuka sana KUIGA, fanya kilicho ndani ya uwezo wako 🙂
3. Cluster of characteristics; hii ni kule kuwa na sifa za ujasilia mali, je wazifahamu? Hizi hapo chini: awe mwenye kutumia fursa zozote zinazojitokeza, awe mwenye kutake RISK ila iwe ndani ya uwezo wake, awe na sifa ya uongozi, awe mwenye kuangalia siku zijazo (future), awe mwenye kukubali makosa na kubadilika, mwenye kujifunza vitu vipya, mwenye kuuliza asipojua na mengineyo!
Kwa mambo hayo kuanzia mtu yeyote aweza kuwa mjasilia mali ila anachotakiwa ni KUJITOA na mwenye UTAYARI wa kufanya jambo, haya ndugu zanguni karibuni kwa wenye mawazo na mjifunze ujasilia mali, PAMOJA TUNAWEZA.
Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums