Mimi nachoweza kusema aliyeruhusu wanyamapori kuuzwa atenguliwe na afunguliwe mashitaka

Mimi nachoweza kusema aliyeruhusu wanyamapori kuuzwa atenguliwe na afunguliwe mashitaka

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2020
Posts
7,899
Reaction score
10,415
Hawa wanyamapori ni urithi wa Taifa letu.

Hivyo ingekua vizuri walioruhusu kuwauza wanyamapori wachukuliwe hatua, watolewe kwenye hizo nafasi wawekwe watu wenye weledi na wanaotambua umuhimu wa wanyapori katika uchumi endelevu kwa taifa. Sii hivyo tu wafunguliwe kesi za uhujumu uchumi endelevu.

Tukiweka mazingira mazuri ya kuvutia watalii, tutaingiza pesa nyingi sana.

Mfano tumwombe Christiano Ronaldo aje Tanzania apige picha na baadhi ya wanyama kama Pundamilia na Twiga.

Akiposti kwenye page yake ya Facebook na Instagram kila mmoja hapa duniani atawaona wanyama, atatamani aje kuwatazama.

Pia kuna wanamuziki maarufu kama Ed Sheeran, mpiga gitaa tumchukue aje afanye kama anavyofanya Christiano, tutapata matokeo makubwa tutaingiza pesa nonstop na huo ndio uchumi endelevu.

Tusipende uchumi feki, wanyama wakiisha tutauza nini tena baadaye??? Lazima tuwaze kichumi. Watu mliopewa dhamana ya kuwapreserve hao wanyamapori, hao wanyama mkiwauza wakiisha mtueleze mtapata wapi chanzo kingine cha mapato? Lazima tuwaze kichumi, hiyo inamaanisha wizara ya maliasili haitakua na vyanzo vingine vya mapato, na huo ni uhujumu uchumi.

Njia bora nikuiga wenzetu Rwanda tutafanye uchumi endelevu na utalii tu ndio njia endelevu ya kujiingizia kipato kupitia wanyama bila kuwauza.

Wenzetu Rwanda wameweka pesa kwenye timu za Arsenal na PSG unaona visit Rwanda imagine Messi anapost picha na jersey inasoma Visit Rwanda hapo nyuma kwanini watu wasiende Rwanda kutalii na kutazama wanyama.

Bango kubwa linasoma Emirates na Parc de Prince Visit Rwanda.

Na hizi timu kwenye mitandao zina followers wengi, lazima nao watatamani kwenda kuwatazama hao wanyama. Pesa inayopatikana ni mara nne zaidi ya bei ya mnyamapori.
 
Acheni watu binafsi wauze wanyama waingize kipato. Acheni akili mgando. Wanyama wa mbugani hawaguswi.
 
Kuna watu ni wajinga sana nchi hii. Wanawaza matumbo yao tu. Sasa tunauzaje wanyamapori? Ili miaka ijayo foreigners wasije Tanzania kutazama hao wanyama? Waende huko tulikouza?
Hivi inakuwaje mtu anajawa na tamaa hadi anashindwa kuona umuhimu wa vizazi vijavyo?
 
Acheni watu binafsi wauze wanyama waingize kipato. Acheni akili mgando. Wanyama wa mbugani hawaguswi.
hao si wenyewe kwa wenyewe?hayo makampuni ni ya kwao ndo maana wanafanya wawezavyo.ni wanasiasa wetu hao wenye hayo makampuni na hutasikia hata yakitajwa hadharani ili wananchi wayajue.
 
Acheni watu binafsi wauze wanyama waingize kipato. Acheni akili mgando. Wanyama wa mbugani hawaguswi.
Wauze wanyama wafugwao. Watu binafsi wamewatoa wapi wanyama pori kama sio mbugani?
 
Kuna watu ni wajinga sana nchi hii. Wanawaza matumbo yao tu. Sasa tunauzaje wanyamapori? Ili miaka ijayo foreigners wasije Tanzania kutazama hao wanyama? Waende huko tulikouza?
Hivi inakuwaje mtu anajawa na tamaa hadi anashindwa kuona umuhimu wa vizazi vijavyo?

Kwa nini foreigners wanakuja wakati kwao kuna ma zoo? Marekani, Ulaya kote kuna ma zoo. Lakini wazungu bado wanakuja. Kwa nini?
 
hao si wenyewe kwa wenyewe?hayo makampuni ni ya kwao ndo maana wanafanya wawezavyo.ni wanasiasa wetu hao wenye hayo makampuni na hutasikia hata yakitajwa hadharani ili wananchi wayajue.
Siyo yote. Kuna wengine ambao sio wanasiasa
 
magu tu aliwapeleka chato mambwa yakapiga kelele sana.

haya kazi imeanza.
 
Hv uingie mbugani uchukue Twiga mali ya serikali..umpandishe kwenye ndege bila kibali kutoka juu..huo utakuwa ni ujasiri wa sayari nyingine sio hii tuliopo..
 
Back
Top Bottom