Mimi naona Kuna wakati mambo yanakuwa magumu kwa kujitakia sisi wenyewe

Mimi naona Kuna wakati mambo yanakuwa magumu kwa kujitakia sisi wenyewe

Joined
Jul 8, 2024
Posts
24
Reaction score
47
Ugumu wa mambo upo kwa kila mtu,

Na kila mtu kwa wakati wake,

Lakini,

Mwitikio kwenye huo ugumu unatofautiana kati ya mtu na mtu,

Na hili ndilo linaamua kujichelewesha au kupita na kushinda licha ya ugumu,

Haya ni baadhi ya mambo mara kwa mara naona hata kwangu huwaa ni sababu ya kufanya ugumu uwe wa muda mrefu,

1. Lawama.

Kwa yeyote yule au hata vitu

Kwa nini wakati wowote tu wa kutoa lawama ni kwamba "wewe hauna nguvu"

Hauna uwezo wowote wa kufanya lolote lile kwenye hilo unapitia

Na hivyo "unamlaumi huyo ambaye" hajafanya sehemu yake,

Yaani una mpa nguvu juu ya utatuzi wa shida zako mwenyewe,

Akifanya unafurahia

Na asipofanya unalaumu sana kwa sababu "hujakubali kiwajibika na maisha yako"

Mara kwa mara ninapojikuta namlaumu mtu yeyote,

Hata kama ni moyoni tu,

Huwa najisemea "Yani unalaumu kama vile huna uwezo wa kufanya maamuzi?"

Unapoacha kulaumu ni kwamba unakubali wewe ndiye dereva wa maisha yako

Ni wewe unaamua mwisho wako uweje

Na hivyo kwa lolote linalotokea unakubali kuwajibika na sio kuwapa watu wengine nguvu au nafasi ya kuwajibikia maisha yako.

2. Woga!

Unajua nini,

Ile hali ya kujiuliza "Vipi kama nitakosea?"

Na mengine mengi,

Nakumbuka niliangalia mazungumzo ya Hanscama kwenye podcast ya msasa Youtube

Na akasema hivi "Usitafute kuwa sawa bila kushughulikia kile kinachokufabya usiwe sawa"

Yani,

Wengi huwa tunaogopa kuchukua hatua fulani ili kubadilisha mambo,

Mfano,

Mimi nimepitia tatizo la kuwa na hela na kisha baadae hela kuisha na hata sielewi zimeishaje,

Sasa,

Ninapopata pesa na kufikiria kuzalisha pesa bado nabaki na woga kwamba vipi kama nitapoteza pesa hizi,

Sasa ili kuondoa woga ninaweza kwenda na kuangalia video za kutia moyo na zakuzema "usiogope"

Fanya "meditation"

Au ni kwamba sasa hivi ninaongeza umakini na kuhakikisha napata uzoefu ili kila senti izae na nisipoteze pesa

Njia ya pili "kuongeza umakini" ni bora zaidi kuliko njia ya kwanza ya kutaka kushughulikia woga kwa kujiambia "siogopi"

"Naweza!"

"Naweza!"

Na usifanye lolote lile kubadilika.

3. Kusubiri "MUNGU" abadilishe maisha yetu,

Kuna wengi waenda kanisani wanabaki kuamini kwamba,

Kwa sababu tu wanaenda kanisani basi "Mungu atawasaidia kubadilisha maisha yao"

Na hata kubaki na kujiuliza "Mbona mimi naenda kanisani kila siku na bado nina maisha magumu?"

Mbona wengine hawasali na wanafanikiwa?

Ni kama hawapitii changamoto kama zangu?

Mpendwa ni hivi,

Swala la kushinda kwenye magumu linategemea sana kanuni,

Na ujue nini hata kabla hunaomba Mungu akusaidie kushinda tayari amekupa uwezo ndani yako wa kushinda,

Lakini ni kwa nini unabaki kusubiri Mungu afanye?

Yote ni kwamba umeaminishwa wewe ni dhaifu na mnyonge,

Inabidi umshawishi Mungu kwa namna fulani ili akubariki uwe kama wengine,

Mh!

Na zaidi kumbuka hili kama ambavyo ukirusha jiwe na linaanguka chini,

Ndivyo ilivyo kwenye "ugumu ambao unapitia" kuna kanuni zinazoongoza kushinda ugumu huo,

Na hata kama unaomba kwa Mungu wako vipi

Bado tu utabaki kukwama,

Hao unaowaona ni kama hawaombi,

Hawaendi kanisani wengi wao ni kwa sababh wanazingatia hizi kanuni za asili na hata bila ya wao kujua,

Na mambo yao yanaenda shwari

Ni bora zaidi baada ya kuomba,

Jiulize "je ni kanuni gani za asili unazivunja na ndio maana unabaki hapo hapo?"

Na kama bado huelewi kanuni hizo,

Mwangalie huyo ambaye unamtuhumu "ni mpagani"

Jilinganishe na wewe

Kisha angalia yeye alipokuwa kwenye tatizo kama lako alifanya nini?

Angalia hatua kwa hatua kile alifanya na jifunze kwake.

Mwisho utaona kwamba kuna tofauti mkubwa,

Ndio maana hata biblia haikuishia kusema "Ombeni..." ila iliendelea kusema "Tafuteni..." , "Bisheni".

Zaidi ya yote kumbuka,

Hakuna ugumu ambao unadumu ila mara nyingi sisi tunajichelewesha kutoka

Unadhani ni sababu ipi nyingine inafanya kutoshinda magumu?
 
MUNGU anawabariki wenye juhudi na sio kusubiri muujiza bila kujishughulisha!

Mfano
Jacob alichunga mbuzi kwa miaka 14, licha ya MUNGU kumuahidi BARAKA!

Tofauti na leo watu wanapingwa sana, bila kujua maandiko!
 
Kuna hoja unaielezea mkuu ila uandishi huo na hii weekend, unanikosesha madini makusudikali!

DOse dose!
 
Back
Top Bottom