Mimi ndio boss we mfanyakazi unataka haki sawa ufanane na mimi

Mimi ndio boss we mfanyakazi unataka haki sawa ufanane na mimi

Annonymous

JF-Expert Member
Joined
May 9, 2013
Posts
688
Reaction score
1,126
POVU: KUNA KIMTU KIMENIKERA ASUBUHI ASUBUHI

Kuna kamtu kananiletea hoja za haki sawa. Yaani katoto ka 2003, ana miaka 20 kasoro miezi kadhaa kananihangaisha mzee mkubwa na ndevu zangu.

Yani nikaajiri, kasifanye kazi nnayotaka, kajipangie siku za kuingia kazini na muda wa kutoka halafu nikanyamazie eti mbona boss wewe siku zingine unachelewa kazini au unawahi kuondoka.

Yaani kazi yangu halafu kamfanyakazi kanipangie. Kamekurupukia haki sawa hata hakaelewi.

Boss nimesema hivi, haki sawa kwangu HAPANA kubwa tena kama ni mwanamke usitegemee kabisa upendeleo kwangu.

Mimi kitu kinaitwa HAKI SAWA ukishaniletea hizo hoja tu jua umeshaacha kazi na nimeshaku disqualify katika kila jambo na nakuona huna akili umejaza kachumbari na nyanya chungu kwenye kichwa.

Wanawake achaneni na suala la haki sawa, litawaondoa kwenye mambo ya msingi na mtaangamia. HAki sawa mpaka Yesu anarudi halitakuja kutimia na litabakia kuwa dhana (concept) kwasababu NATURE haiko katika haki sawa na haihamasishi haki sawa.

NATURE IS NOT EQUALIZED AND NOT INFLUENCING EQUALITY. NATURE HAS EQUITY AND NOT EQUALITY
 
amna boss apo na wewe hio sio fani yako, yani muajiriwa anaanzia wapi kuomba haki sawa kama hajakudharau.
 
Hiyo ni Kaz ya m pesa au, ungeleta Uzi apa kuwa ushamap red card ,
Wala hayo maelezo mi nisingempa ningemwambia Lete funguo tu,
 
Ukishaona mtu anajiita bocy kwa majigambo, ujue siye Bocy
 
Wewe utakuwa boss wa mchongo tu. Boss gani anakuja kulalamika JF issue ndogo kama hiyo? Hapo ilitakiwa uwe umechukua hatua kitambo halafu unatulia zako tuliii.
 
Kwaio bosi na stafu mnarushiana vijembe status?
Itakua hyo ofisi ni ya kuuza vitenge na vigodoro..
 
Boss unakuja kulalamika JF ili usaidiwe nini?

Halafu kwenye bandiko lako kuna sentensi ya kuwanyanyapaa wanawake.
 
Back
Top Bottom