Vien
JF-Expert Member
- Mar 6, 2020
- 8,508
- 15,276
Kuna siku nilikaa nikamtazama mwanangu kwa makini sana.
Sio tu sura.
Sio tu macho.
Sio tu tabasamu.
Tabia.
Misimamo.
Namna anavyoongea.
Namna anavyojibu watu.
Hata namna anavyokasirika.
Nilicheka kimya kimya nikasema, “Huyu ni mimi kabisa.”
Nilimkumbuka mama yake. Tulikutana mwaka 2015.
Haikuwa relationship ya muda mrefu sana, lakini ilizaa matokeo makubwa zaidi ya tulivyotarajia - ujauzito.
Wakati huo tulikuwa vijana.
Hakuna aliyekuwa amejiandaa kikamilifu kuwa mzazi.
Lakini maisha hayangoji mipango yetu ikamilike.
Miaka imepita.
Kijana wangu sasa amekua.
Na kila ninapomuangalia, naona mfano halisi wa mchango wangu ndani yake.
Na hapo ndipo nikapata mfano huu wa rangi.
Kwenye kuchanganya rangi, unakuta kuna base tayari imeandaliwa.
Base peke yake ina muonekano wake, lakini haina muelekeo kamili wa rangi unayotaka.
Kisha unaongeza toner.
Na toner ndio inaipa rangi identity yake halisi.
Inaipa mwelekeo.
Inaipa tabia.
Inaipa final touch.
Na nilipomtazama mwanangu, nikatabasamu nikasema, “Mimi ndo niliyetoa toner. Kwa mama yake nilifuata base tuu.”
Lakini nisieleweke vibaya.
Base ni muhimu.
Bila base hakuna pa kuweka toner.
Bila mama yake, asingekuwepo kabisa.
Lakini kuna vitu ambavyo huwezi kuvificha.
DNA inaongea.
Tabia zinaongea.
Msimamo unaongea.
Mtoto wangu anavyopenda kuchunguza vitu, ni mimi.
Anavyokataa kuonewa, ni mimi.
Anavyotaka kujitegemea, ni mimi.
Hata namna anavyopenda kukaa kimya akiwaza, ni mimi kabisa.
Hapa ndipo unagundua kitu kikubwa kwenye mahusiano na uzazi.
Wakati mwingine relationship inaweza isidumu.
Lakini matokeo yake yanadumu milele.
Unaweza usiendelee na mama wa mtoto.
Lakini sehemu yako ndani ya mtoto haiwezi kufutika.
Na kuna fahari fulani inakuja pale unapoona mchango wako unaishi mbele yako.
Sio kwenye pesa tu.
Sio kwenye sura tu.
Bali kwenye maadili, misimamo na mtazamo wa maisha.
Lakini pia kuna wajibu mkubwa sana.
Kwa sababu kama kweli wewe ndiye “toner,”
basi hakikisha rangi unayoiacha ndani yake ni sahihi.
Hakikisha tabia zako ni za kuigwa.
Hakikisha misimamo yako ina msingi.
Hakikisha uwepo wako kwenye maisha yake ni wa kujenga, sio wa kujionyesha.
Kwa sababu siku moja atakua mwanaume kamili.
Na watu watamuona yeye - lakini watasoma wewe ndani yake.
Mwisho wa siku, uzazi sio mashindano ya nani amefanana naye zaidi.
Ni jukumu la kuhakikisha huyo mtoto anakuwa bora kuliko sisi wote wawili.
Lakini niseme tu ukweli…
Nikimtazama mwanangu leo, naona signature yangu waziwazi.