Mimi ni kijana ninayeelekea miaka 27; kutokana na ratiba zangu, ni wazi kuwa ratiba inayofuata ni ndoa

Mimi ni kijana ninayeelekea miaka 27; kutokana na ratiba zangu, ni wazi kuwa ratiba inayofuata ni ndoa

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Hello habari,

Natumai upo salama. Mm Mimi ni kijana wa miaka 26 now naelekea 27, na kutokana na ratiba zangu, ni wazi kuwa ratiba inayofuata ni ndoa.

Nimebakiwa na mzazi wa kiume. Kwa hivyo, nikaona siyo mbaya kama mzazi basi acha nimshirikishe, japokuwa najua kila kitu nitamaliza mwenyewe.

Ila nilipomgusia mzee kuhusu hilo swala bila kumwambia muhusika, mzee alinipa vigezo vya mkamwana anayempenda. Mwisho kabisa, akasema: "Japo sijui status ya huyo mkwe, ila huku sitaki mtu mwenye mtoto. Na ukifanya hivyo, basi tafuta baba yako na pia utafute kwenu, ila hapa marufuku. Haijalishi kazalia nyumbani wala kaachika, ila as long as ana mtoto basi simtaki."

Nilipomuuliza sababu, yeye alinijibu tu kuwa ndiye anayejua wa kwanza, kwa hiyo "akili kichwani mwako!"

Sasa, niliyetaka nimuoe ni binti aliyezalishwa na kijana wa Kikristo, halafu huyo kijana akamkimbia. Huyu binti nimemaliza naye miezi nne. Ila ilibidi tu nimwambie ukweli kuhusu uamuzi wa mzazi wangu. Mwanzoni, alionekana kuukubali ukweli na kunishauri nifuate kauli ya mzazi, ila hivi karibuni ameripuka tu ghafla na kunilaumu kuwa nimemuharibu. Mara aseme nataka kumuacha, mara aseme dunia itanifunza.

Yaani, nachanganyikiwa! Nampenda kweli, lakini wazazi ndio wamegoma. Je, nifanyeje? Na vipi kuhusu kauli za huyu binti kuwa nimemuharibu wakati nilidate naye miezi nne pekee? Maana sijamtoa bikira mm wala sijamzalisha mm, nilimkuta na mtoto wake. Je, nimeharibu nini labda?

MKUSHI: Unampenda binti kabisa au na ww ulikuwa naye mguu pande mguu sawa, hoja ya baba imekuwa kama kishikizo tu?

MUOAJI: Huyu binti nampenda, kwa sababu mbali na kuwa single mother, hajawahi kunigharimu kabisa. In fact, nilitaka ndiye nipeleke posa kwao, na kwao wangetaka wazee upande wangu. Sasa hadi nashindwa nifanyeje!?

1733683974144.jpg
 
Back
Top Bottom