twakuombe mungu akusaidie.
Kama ni Mkristo au wa dini yeyote ile mtumaini Mungu, soma Biblia:
Mithali 19:14 "Nyumba na mali ni urithi apatao mtu kutoka kwa babaye bali mke mwenye busara mtu hupewa na Bwana'
Kwa MUNGU: mume mwenye busara mtu hupata kutoka kwa Bwana, maana yake Mungu ndiye anayehusika na kumpa mtu mke/mume. Mungu pekee ndiye anayejua nani ana busara ya kukaa nawe. Kwa kila jambo kuna majira yake hivyo hata wewe kuolewa kwako kuna wakati wako maalumu. Mungu hatumii njia au mfumo wa aina moja katika kukujulisha wewe mwenzi wako.
Mungu anavyo vigezo vya kwake ya kukupa mume ambavyo si lazima viendane na vigezo vya kwako.
Si kila mke au mume hutoka kwa Mungu. Mungu anapoamua kukupa mke au mume anakuwa ameangalia mbali kuliko wewe unavyofikiria.
USIKATE TAMAA, ENDELEA KUOMBA MUNGU UTAPATA MAJIBU KIPINDI KIKIFIKA.