Mimi ni Mtanzania Bara nasema muungano uvunjwe.

Mimi ni Mtanzania Bara nasema muungano uvunjwe.

mkigoma

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2011
Posts
1,180
Reaction score
309
Huu si muungano Bali ni dhulma za wazi kabisa upande mmoja dhidi ya upande mwingine wa muungano, kwanini tuendelee kuwadhulumu? Tusivunje muungano kila upande uendeshe mambo yake? Tumeunda tume tupate maoni ya wanainchi, wametaka serikali tatu CCM hawataki, hii ina maana gani kama sio CCM kuendeleza dhulma dhidi ya Zanzibar kwa kuwatumia vibaraka wachache walioko huko, nasema Kama tume watanadili maoni ya wanainchi bora muungano ufe
 
Mimi ni Mtanzania Bara nasema muungano uvunjwe.

Mimi nafikiri jambo la msingi siyo kuuvunja au kutokuuvunja huo unaoitwa muungano, bali ni kuthibitisha kwanza kama huo muungano wenyewe ulishawahi kuwepo. Maswali yafuatayo ni lazima yajibiwe kwanza:

1. Tunazo serikali mbili, serikali ya mapinduzi zanzibar na serikali ya muungano. SWALi: Ina maana zanzibar imeungana na serikali ya muungano? au imeungana na nini?

2. Zanzibar inaye Rais wake anayekanyaga zuria jekundu na kupigiwa saluti na mizinga, Bunge lake, Jeshi lake, Wimbo wake wa taifa, Vitambulisho vyake vya mzanzibari mkazi, mfumo wake wa kodi, mkuu wa jeshi la polisi zanzibar, na kama sikosei inadai bendera yake na wimbo wake wa taifa. Sasa ni kitu gani Zanzibar inachopungukiwa hata isiwe ni Taifa? Je Tanganyika ina nini?

Sasa tusijeng'ang'ania kuuvunja muungano kumbe muungano wenyewe haupo. Tunaomba wanasheria watusaidie.
 
Muungano umekufa tokea alipokufa maremu tanganyika.
 
Back
Top Bottom