Mimi ni mtoto wa mama, kula kulala, nina mika 40 na ninataka kuoa

Mimi ni mtoto wa mama, kula kulala, nina mika 40 na ninataka kuoa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Wana JF Heri ya mwaka mpya.

Mimi ni baba wa miaka 40 form four leaver, sina ujuzi wala maarifa yoyote ya maisha. Tangu nimalize elimu ya sekondari, sijawahi kufanya kazi yoyote ya kuniingizia kipato. Sijawahi kutengeneza pesa yangu mwenyewe. Kila hela unapewa na mama, hata hela ya kununua boksa.

Sijawahi kupanga wala kuishi maisha ya kujitegemea. Nimeshakuwa kwenye mahusiano ya ki mapenzi na wasichana wengi wasio na idadi, ila sikuwahi kufikiria kuoa. Nina watoto wawili, nilizaa na wasichana tofauti, watoto wanaishi na mama zao.

Kilichonisukuma kuandika uzi huu, ni kwamba kuna Dada nimempata, na nimetokea kumpenda kwa dhati. Nimemuahidi kuwa ntamuoa.

Sasa mchumba wangu huyo anataka nikapange, nianze kujitegemea?

Jamani wazoefu wa maisha naomba mnipe mbinu za kutafuta hela niache kumtegemea mama na Mimi niweze kama wanaume wengine .

Nawashukuru sana.

Vijana kula kuwala watoto wa mama tuko wengi sana DSM, ila Mimi nimejitokeza hadharani. TID ni mwenzangu pia, Toto la mama.
 
Nenda sokoni,
Kaombe kazi ya kutembeza matunda.

Per day utaingiza hadi elfu 15.
Ganji elfu 8, malipo per day elfu 7.

Kwa mwezi laki 4 na nusu, maisha safi kabisa.

Mama akikupa mtaji wa tololi peke yake itapendeza zaidi.
 
Back
Top Bottom