Mimi ni Mzalendo sana. Ila katika hili mimi nimeshindwa kabisa

Mimi ni Mzalendo sana. Ila katika hili mimi nimeshindwa kabisa

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Mimi Mzalendo sana tu. Ila ukiniambia nivae nguo yenye mirangi ya bendera yetu ntakukatalia mpaka mwisho. Bendera yetu ina mirangi mibaya. Haipendezi kwenye tai wala jersey. Kwenye tai labda iwe tu Blue au Nyeusi pekee.

Lakini eti univalishe li tshirt,tai au bendera yenye ile mirangi. Hapana..imefubaa sana. Ndo maana naona hata mambo mengi yamefubaa. Akili za watu wengi zimefubaa, uchumi umefubaa....

Yaani unaona tu kila kitu ni shida pengine na ile mirangi nayo inachangia. Halafu ukiwashwa na mwenge unawamulikia watu wa nje waone nafasi zilizomo ndani na mali zetu. Waje wazichukue. Sisi tunavuta moshi unaingia kwenye ubongo unafubaza akili.

Tunakufa huku tunatembea ndo maana hata mwenye bendera kuna rangi ya kaniki. Ile ni ya kuonesha kuwa sisi tuna kiza. Tutakufa tu tuzikwe majani na miti viote juu yetu. Ndo rangi ya kijani. Ivutie watu.

Pia tutakapozikwa tunatoa madini ndo hayo wanakuja vuna wazungu,wachina na wengine. Halafu sisi tunabaki kizan. Umeme hakuna na maji hakuna. Mimi hunivalishi hayo marangi. Nabaki kuwa Mzalendo wa Nchi yangu mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom