SoC02 Mimi ni Sayari

SoC02 Mimi ni Sayari

Stories of Change - 2022 Competition

Dunia Mwalukasa

New Member
Joined
Aug 26, 2022
Posts
4
Reaction score
2
Hata kulalamika kwamba umeme unakatika kila siku wakati hata ule kidogo uliopo unautumia kuchajia simu ni kufikiri ndani ya kasha. Wachina wanautumia umeme kubadili usiku kuwa mchana ili wafanye kazi sisi tunautumia umeme kuchaji simu ili tusikose kuchat. Umeme ukikatika tunawatukana TANESCO wametukatiri kumalizia ile tamthiliya ya kifilipino. Bora basi tungekuwa tunautumia umeme kutengeneza hata barafu.

Kutofanya lolote ni uvivu. Uvivu husababisha umaskini. Uvivu ni mama wa njaa imeandikwa katika Torati. Mpe kazi ili asiwe mvivu, maana uvivu huwafunza watu uovu mwingi alisema Sira. Wazungu wanasema, “An idle mind is the devil's workshop.” Yaani shetani atakupa kazi.

Mwanaume mmoja alikwenda kwa mchawi kutafuta utajiri. Yule mchawi akamwambia aende na mkewe. Walipofika, mchawi akasema, “Mwanaume aingie kwanza.” Alipoingia mchawi alifunga mlango na kuanza kumchanja kwa wembe na kumpaka pilipili. Jamaa alipiga yowe kwa maumivu aliyoyapata.

Baadaye alimwambia atoke nje mke wake aingie. Mke wake alipoingia mchawi alifunga mlango na kuanza kumbaka. Mwanamke alipiga kelele. Mume wake alifikiri sasa anapakwa dawa yenye pilipili kama alivyopakwa yeye. Hivyo alimwambia mke wake, “Vumilia, tulia, jikaze mke wangu.”Mke wake alifikiri kuwa mume wake ametoa kibali abakwe kama sehemu ya dawa ya utajiri.” Shetani aliwapatia cha kufanya.

Hiyo ndio faida ya kukaa bila kufanya lolote maana shetani anakupa la kufanya. Unapokuwa busy na kazi, huwezi kupata muda wa kutenda ovyo. Watoto wetu wanafanya mambo ya ovyo na sisi tunaishia kuwaita kizazi cha nyoka. Kosa ni letu wazazi. Hatujawapa kazi.

Zamani baada ya kutoka shuleni tulikwenda kuchunga mbuzi. Siku hizi baada ya masomo watoto wetu wanakwenda kuchunga rimoti na simu za tachi. Watoto wanadekezwa mpaka hata kufua nguo zao za ndani hawajui. Anafua housegirl. Hatujui kama kufanya hivyo ni kumpa shetani nafasi awashughulishe.

Sababu kubwa inayotufanya tuendelee kuishi huku tukivumilia maumivu sio ung`ang`anizi bali ni kutafuta nafasi moja itakayobadilisha maumivu yetu kuwa Furaha na faraja Lakini pia kutafuta nafasi ya kuwafariji wengine wanaopitia maumivu.

Hatuna kinyongo na mtu kwa sababu Furaha iliyopotea maishani mwetu haikusababishwa na watu Bali ilisababishwa na nafasi tulizozikosa na Kama tutazipata Mambo hayatabaki Kama yalivyo.

Sisi sio watu wa kawaida na tena licha ya kuwa tuna mapungufu mengi sana, bado Kuna watu wengi wanaotupenda daima, kutufuata na kuendelea kuwa upande wetu.

Maumivu ya kudharauliwa na wale tunaowahitaji yanatufanya tuwashikilie maradufu wale wanaotuhitaji licha ya kuwa hatuna kitu Cha kuwapa.

Licha ya kuwa sisi ni watu wanaopambana kutoka chini, bado Hali hii haitufanyi tukakosa imani ya kufanikiwa kiasi Cha kukufuru.

Zile nafasi ambazo tulizichezea na zikatupita sio kwamba ndio zilikuwa dhahabu pekee ya kufanikiwa kwetu, tuna Imani katika mapambano ambayo jasho lake haliwezi kumtupa mja

Sisi ni Dunia isiyoishiwa kiu ya kuwa Bora zaidi na ubora wetu haupo katika kulipiza mabaya kwa waliowahi kutufanyia mabaya na Tena ubora wetu haupo katika kuwachafua wale waliowahi kutuchafua Tena ubora wetu haupo katika kuwachukia waliotukosoa.

Tumejengeka Sana katika uvumilivu, subira, kufanya kazi kwa bidii na kukaa kimya wakati
tunapotambua nafasi ya maneno yetu katika kukosana na ndugu na marafiki zetu.

Hii Ni siku nyingine Tena na wacha tukapambane Sana.

Tunajua Watoto wetu watatamani kuona matokeo kuliko mipango isiyo fanyiwa kazi, watatamani kuona maisha mazuri, Watatamani kupata mahitaji yao muhimu kutoka kwetu hivyo kila kitu kinachoweza kutuweka katika nafasi ya kuwakosesha watoto wetu watakaokuja Mambo hayo tunakikata mapema.

Tunajiamini sio kwa sababu ya nguvu, au majeshi au vyeo vya nyota tulizonazo Bali tunajiamini kwa sababu MUNGU yupo upande wetu na zaidi Kupitia Yeye Hakuna aliye juu yetu.

Karibu katika ulimwengu wa mafanikio na changamoto.
Dunia Mwalukasa
0759474686
duniamwalukasa@gmail.com
MBEYA.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom