RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
HOTUBA YA VIRUSI VYA UKIMWI (MTOTO PEKEE WA KIUME WA MZEE UKIMWI)
VVU amesimama jukwaani mbele ya wanadamu, anasema;
"Najua mnanijua ila leo nataka mnijue zaidi. Watu wengi huko mitaani wamenipachika majina ya utani wananiita miwaya, taa, ngoma, kisiki, gonjwa kubwa, na majina mengine mbalimbali. Hayo si majina yangu halisi, jina langu halisi na la ubatizo ni VVU - mtoto pekee wa kiume wa mzee UKIMWI.
Baba yangu anaitwa UKIMWI, ndiye aliyenituma leo nisimame mbele yenu niongee na nyinyi wanadamu. Mwaka 2019 alikuja binamu yangu anaitwa Corona (Covid-19), alinifanya mimi na baba yangu tusahaulike mtaani lakini tulikuwepo na bado tupo.
Samahani kwa hili, lakini nawakumbusha kuwa nimeua wanadamu wengi wa rika lote yaani watoto, vijana na wazee wa jinsia zote, kwasababu mimi ni VVU - ni mtoto pekee wa kiume wa mzee UKIMWI.
Mimi na baba yangu tunaishi maeneo mbalimbali kama vile kwenye kumbi za starehe, makanisani, misikitini, vyuoni, misibani, harusini, mashuleni, vilabuni, sokoni, hotelini, nyumba za kulala wageni, na majumbani mwenu. Nawapenda sana walevi, wahuni wa mapenzi, na malaya kwasababu siku zote hawachukui tahadhali dhidi yangu hivyo nipo nao sambamba kama mstari mnyoofu nahakikisha sikunji kona.
Mimi na baba yangu chakula chetu ni damu. Wewe mwanaume ambaye hupitwi na wanawake wenye makalio makubwa na mishangazi, na wewe mwanamke unayependa ngono kwa wazee ambao mnawaita "mubaba" kwasababu ya pesa, nakukumbusha kuwa mimi ni VVU - mtoto pekee wa kiume wa mzee UKIMWI.
Sipo hapa kwa ajili ya kujisifu, bali nipo kwa lengo la kuwakumbusha nyinyi wanadamu kuwa mimi bado nipo mtaani nadunda. Nimetumwa na baba yangu mzee UKIMWI niwawinde watu wa rika lote kwa maana ya watoto, vijana, wazee, na wanawake kwa waume. Sitanii nakuahidi nikikupata nitakuadhibu ipasavyo, na usipozingatia ushauri nasaha wa madaktari hakika nakueleza wazi nitakubakisha skeleton tu, kwasababu mimi ni VVU - mtoto pekee wa kiume wa mzee UKIMWI.
Zipo njia kadhaa za kuniepuka mimi na baba yangu mzee UKIMWI. Njia hizo ni kama vile; matumizi sahihi ya kondomu, kuacha kushiriki ngono na wapenzi wengi, kuwa mwaminifu katika ndoa au uhusiano wako, kutochangia vifaa vyenye ncha kali, kupima afya mara kwa mara, na njia nyingine nyingi. Lakini kubwa zaidi ni kumrudia Mungu wako, ukipuuza hayo yote nakuahidi siku moja nitakukamata kwasababu mimi ni VVU - mtoto pekee wa kiume wa mzee UKIMWI.
Nashukuru sana kwa kunisikiliza. Naomba nitoe pole kwa wale wote wanaoishi namimi katika maisha yao, wasikate tamaa kwasababu kama watazingatia ushauri nasaha wa madaktari pamoja na kumuabudu Mungu, hakika mimi sitoweza kuwaadhibu. Mwisho kabisa nawakumbusha jina langu; naitwa VVU - ni mtoto pekee wa kiume wa mzee UKIMWI".
Imeandikwa na;
RIGHT MARKER,
Dar es salaam.