Mimi niko (Mama yake)

Mimi niko (Mama yake)

ward41

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2022
Posts
749
Reaction score
2,533
1000137002.jpg


Mungu alijitambulisha kwa MUSA kwamba yeye anaitwa " MIMI NIKO"
Kutoka 3:14

MINI MAANA "MIMI NIKO"?
Haya maneno asili yake ni lugha ya kiEbrania "Ehyeh Asher Ehyeh"

Nini maana ya Ehyeh Asher Ehyeh
Hayo mane no Yanamaanisha "Self Sufficient" au Anaejitosheleza.

Haya ni maneno mazito Sana. Mwenye hizo sifa ni Mungu tu

Maneno hayo tunaona Yesu anajitambulisha kwa waYahudi.
Yohana 8:58.

Yesu alijitambulisha kwa hayo maneno kwamba "Mimi NIKO"
Yesu ni self sufficient, yaani Ananitosheleza. Au kwa lugha nyingine YESU ni Mungu
 
View attachment 3172997
Mungu alijitambulisha kwa MUSA kwamba yeye anaitwa " MIMI NIKO"
Kutoka 3:14

MINI MAANA "MIMI NIKO"?
Haya maneno asili yake ni lugha ya kiEbrania "Ehyeh Asher Ehyeh"

Nini maana ya Ehyeh Asher Ehyeh
Hayo mane no Yanamaanisha "Self Sufficient" au Anaejitosheleza.

Haya ni maneno mazito Sana. Mwenye hizo sifa ni Mungu tu

Maneno hayo tunaona Yesu anajitambulisha kwa waYahudi.
Yohana 8:58.

Yesu alijitambulisha kwa hayo maneno kwamba "Mimi NIKO"
Yesu ni self sufficient, yaani Ananitosheleza. Au kwa lugha nyingine YESU ni Mungu
Exodus 3:14 (KJV) And God said unto Moses, I AM THAT I AM: and he said, Thus shalt thou say unto the children of Israel, I AM hath sent me unto you.
 
Ufafanuzi mzuri...
1. Nipo ambaye nipo
2. Nipo niliyekuwepo
3. Nipo nitakaye endelea kuwepo
 
Nabii Isaya pia alitoa unabii kuwa MIMI NIKO atakuja duniani kuongea na watu wake.

Isaya 9:6
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa,
Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake;
Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu,
Mungu mwenye nguvu,
Baba wa milele,
Mfalme wa amani.

Mwanafunzi wa Yesu Yohana alifunuliwa pia jambo hili.

Yohana 1:1
Hapo mwanzo kulikuwako Neno, naye Neno alikuwako kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu.
2 Huyo mwanzo alikuwako kwa Mungu.
3 Vyote vilifanyika kwa huyo; wala pasipo yeye hakikufanyika cho chote kilichofanyika.
4 Ndani yake ndimo ulimokuwa uzima, nao ule uzima ulikuwa nuru ya watu.
5 Nayo nuru yang'aa gizani, wala giza halikuiweza.
6 Palitokea mtu, ametumwa kutoka kwa Mungu, jina lake Yohana.
7 Huyo alikuja kwa ushuhuda, ili aishuhudie ile nuru, wote wapate kuamini kwa yeye.
8 Huyo hakuwa ile nuru, bali alikuja ili aishuhudie ile nuru.
9 Kulikuwako Nuru halisi, amtiaye nuru kila mtu, akija katika ulimwengu.
10 Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua.
11 Alikuja kwake, wala walio wake hawakumpokea.
12 Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake;
13 waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu.

14 Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; nasi tukauona utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee atokaye kwa Baba; amejaa neema na kweli.
 
Back
Top Bottom