MIMI : Nikuulize jambo, askofu? ASKOFU: Ndio, uliza mtumishi wa Baba πŸ˜€.

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
2,858
Reaction score
5,123
MIMI : Nikuulize jambo, askofu?

ASKOFU: Ndio, uliza mtumishi wa Baba
πŸ˜€.

MIMI: Hivi kati ya Mungu na nyoka nani
aliyemdanganya Mtu pale
β€Žbustanini?

ASKOFU: Nyoka ndo alindanganya
mwanadamu. Mungu
β€Žalimwambia mwanadamu kuwa
β€Žakila atakufa. Ila nyoka
β€Žakamdanganya kwamba akila
β€Žatafanana na Mungu.

MIMI: Mbona unaanza tena
kunidanganya, baba askofu! Ndo
β€Žimeandikwa hivyo kwamba
β€Žatafanana na Mungu?

ASKOFU: We kijana vipi? Hujui ndo
imeandikwa hivyo? Imeandikwa
β€Žkuwa akila atafanana na
β€ŽMungu.

MIMI: Hebu Nisomee hilo fungu
tuonehilo fungu tuone.

ASKOFU: biblia katika Mwanzo 3:4
Inasema "Nyoka akamwambia
β€Žmwanamke, Hakika hamtakufa,
β€ŽMwanzo 3:5
kwa maana Mungu anajua ya
β€Žkwamba siku mtakayokula
β€Žmatunda ya mti huo,
β€Žmtafumbuliwa macho, nanyi
β€ŽMTAKUWA KAMA MUNGU,
β€Žmkiju mema na mabaya.

MIMI : Mbona sijaona palipoandikwa
kuwa watafanana na Mungu?

ASKOFU: Ndio, hapapo. Ila kuwa kama
Mungu ndo tulifundishwa tuwe
β€Žtunaitafsiri kama kufanana na
β€ŽMungu.

MIMI: Kwani Mwanzo 1:26 si inaonesha
kuwa Mungu alikuwa na agenda ya
β€Žkumuumba mtu kwa mfano wao?
β€ŽMbona hapa nyoka anasema
β€Žwatakuwa kama Mungu? Ina
β€Žmaana Hawakuumbwa kwa mfano
β€Žwake?

ASKOFU: Hapo sasa ndo utaanza kuona
uongo wa nyoka hehehee. Yaani
β€Žhapa bila macho ya kiroho
β€Žhuwezi kuelewa. Ila tayari roho
β€Žameanza kukuelekeza kwenye
β€Žukweli. Nyoka ni Muongo maana
β€Žtayari Mwanadamu alikuwa
β€Žameshaumbwa kwa Mfano wa
β€ŽMungu. Kwa hiyo kwa kula tunda
β€Žasingeweza kuwa kama Mungu.

MIMI: Kwa hiyo nyoka alidanganya kwa
kumwambia Mtu kuwa Atakuwa
β€Žkama Mungu akijuwa mema Na
β€Žmabaya?

ASKOFU: Haswaaa.. Nyoka ni Muongo na
alidanganya. Mwanzo 3:5
[5]kwa maana Mungu anajua ya
β€Žkwamba siku mtakayokula
β€Žmatunda ya mti huo,
β€Žmtafumbuliwa macho, nanyi
β€ŽMTAKUWA KAMA MUNGU
β€ŽMKIJUWA MEMA NA MABAYA.

MIMI: Hebu nisomee Mwanzo 3:22.

ASKOFU: Haya sawa, hehehehee.
Mwanzo 3:22 NENO LA BABA
β€ŽYETU LINASEMAH,

MIMI: LINASEMA NINI?

ASKOFU: [22]BWANA Mungu akasema,
Basi, huyu mtu ANEKUWA
β€ŽKAMA MMOJA WETU, AKIJUWA
β€ŽMEMA NA MABAYA; na sasa
β€Žasije
β€Žakanyosha mkono wake
β€Žakatwaa matunda ya mti wa
β€Žuzima, akala, akaishi milele;

MIMI : Mbona Mungu hapa
anakiri usahihi wa Kauli ya
β€Žshetani
β€Žkwa kuonesha kabisa kuwa ni
β€Žkweli mtu angekuwa kama
β€ŽMungu pindi akila tunda la
β€ŽMema na Mabaya?

ASKOFU: Hakuna kitu hapo, Wewe ndo
huelewi kabisa na tena Omba
β€Žsana Roho akufunulie uweze
β€Žkulijuwa neno la Baba yetu. Ni
β€Žkweli walikuwa kama Mungu
β€Žkwa kujuwa mema na mabaya,
β€Žila sio kufanana naye
β€Žkimuonekano.

MIMI : Kwani shetani alisema kuwa
mwanadamu akila tunda
β€Žatakuwa kama Mungu kwa
β€Žkufanana naye kimuonekano.

ASKOFU: Hujanielewa... Halafu tatizo lako
huna roho ndio maana shetani
β€Žanakufanya uwaze mambo ya
β€Žkijinga mda wote. Hii sehemu ni
β€Žngumu, kijana. Kuielewa ni hadi
β€Žuwe umesoma tioloji kwenye
β€Žvyuo vyetu.

MIMI : Basi hilo swali gumu. Niulize,
Mwanadamu aliumbwa kwa
β€Žmfano wa Mungu?

ASKOFU: Ndio. Mwanadamu aliumbwa
kwa mfano wa Mungu kabisa
β€Žna hilo liko wazi, ama
β€Žnikufungulie vitabu?

MIMI: Tutavifungua tu usijali. Je
alikuwa anajuwa mema na
β€Žmabaya?

ASKOFU: Alikuwa anajuwa mema tu ila
hajui mabaya.

MIMI: Mbona Mungu anakiri
mwenyewe katika Mwanzo 3:22,
β€Žbaada ya yeye kula tunda kuwa "
β€ŽSasa amejuwa mema na
β€Žmabaya?" Huoni kuwa
β€Žmwanadamu bado alikuwa hajui
β€Žmema na mabaya?

ASKOFU: Yeah, nilikuwa nimesahau.
Nisamehe kwa hilo.
Ukisoma kwa umakini unaona
β€Žkabisa kuwa mwanadamu
β€Žalikuwa hajui mema na mabaya
β€Žmaana yalikuwa yamefungwa
β€Žkwenye mti wa ujuzi wa mema
β€Žna mabaya.

MIMI: Sasa kama bado alikuwa hana
ujuzi wa mema na mabaya.
β€ŽAliwezaje kutambua kama Mungu
β€Žanachomuelekeza ni chema. Ama
β€Žnyoka anachomuelekeza ni
β€ŽKibaya na hila?

ASKOFU: Hapa ni wazi kuwa unaanza
sasa kukufuru. Kwa hiyo,
β€Žunataka kuniambia kuwa Mungu
β€Žalimuonea Mwanadamu,
β€Žkwasababu tu
β€Žalimpa
β€Žmaagizo wakati ambapo
β€Žmwanadamu hakuwa
β€Žna utambuzi wa lipi jema ama
β€Žlipi baya? Si ndo hivo?

MIMI: Ndio. Nina mwanangu ana miezi
mitano sasa bado hajawa na.
β€Žutambuzi wa lipi jema na lipi
β€Žbaya. Iwapo nitamuwekea chupa
β€Žya chai mbele halafu nimpe
β€Žmaelekezo kuwa asiishike hiyo
β€Žchupa maana akifanya hivyo,
β€Žitapasuka na ataungua. Je,
β€Žataelewa kuwa maagizo
β€Žniliyompa ni
β€Žmema?

ASKOFU: Hapana. Bado hajapata
utambuzi. Itabidi umlinde sana
β€Žna sio kumpa majaribu. Lakini
β€Žadamu alikuwa
β€Žmtu mzima hata kama hakuwa
β€Žna utambuzi.

MIMI: Kwa hiyo hakupaswa kupewa
ulinzi kamili na kuepushwa na
β€Žmajaribu kama unavyonishauri
β€Žnifanye kwa mwanangu?

ASKOFU: Tunakoelekea sasa tutakufuru
kijana. Staki uje upate matatizo
β€Žkabisa. Utapigwa mapigo
β€Žmabaya na Mungu kama
β€ŽWaliyoyapata wamisri.

MIMI: Sasa mbona badala ya kunijibu
unaanza kunitisha? Kwani huoni
β€Žkuwa Mungu wako aliadhibu
β€Žwatu wazima kwa makosa
β€Žwaliyoyafanya wakati ambapo
β€Žwalikuwa bado wachanga?

ASKOFU: Sawa walikuwa wachanga. Na
waliadhibiwa kwa kuonewa. Ila
β€Žhayo mambo hayamfanyi
β€ŽMungu wetu kuwa muonevu.
β€ŽMungu wetu ana huruma, ana
β€Župendo, na msamaha.
β€ŽJinyenyekeze mbele zake la
β€Žsivyo Siku ya Mwisho
β€Žutaadhibiwa.
β€Ž
MIMI: Kwa hiyo hayo uliyayaona na
uliyoyataja, ni upendo ama
β€Žudhibiti?
Yaani ninakuambia kuwa nina
β€Žhuruma msamaha, upendo na
β€Žsilazimishi. Ila usiponifuata
β€Žnitakuangamiza? Huoni huo ni
β€Žudhibiti na sio uhuru?

ASKOFU: Unatafuta uhuru kwa Mungu, si
ndo hivyo? Acha Niwapigie
β€Žpolisi waje kukupa uhuru kijana.

MIMI: πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡πŸ‘‡
 
Kuna swali nilimuuliza mchungaji faluni
akasema eti mimi ni pepo mchafu nimetumwa kumjaribu

aisee hizi dini!
 
Hapo hapakua na Nyoka wala baba yake Nyoka.
Hapo ilikua ni vuta nikuvute kati ya Shetani [Wale malaika walioasi], wampe Enlightment Mwanadamu, ajitambue zaidi, na ikiwezekana ajue siri zote za uMungu, ulimwengu na yeye ili kwa kujua huko wamuasi Mungu pia.Na ndo maana kwenye vitabu mfano cha Enock ambacho hakikuchapwa kwenye hii biblia, utaona kuna malaika wanafundisha watu elimu zote za dunia hii - kabla ya hapo mwanadamu alikua kama kopo tu, programmed...hujui mema, mabaya, ubaya, wewe ni kula bata tu huku uko restricted.

Hawa jamaa, wakawafundisha wanadamu uchawi, astronomy, sayansi ya vita, utabibu n.k.nk
Ikabaki kidogo tu apate siri ya kuishi milele - Mungu akaona sasa nyie wapuuzi mmezidi ..mnakoelekea mtatengeneza kiumbe ambacho hakitabiriki na kitaleta imbalances.
Mungu kapiga pin, kafungia access ya elimu na utambuzi zaidi...shetani naye akawa restricted...BinAdamu akabaki anababaika, anatangatanga na elimu nusu....hadi leo hatujielewi.

Baadae binadamu walijiorganize tena - ubishi uleule.Kwanza wakawa wanaongea lugha moja maana yake wanashare mambo...UMOJA NI NGUVU, pili wakataka kumchallenge Mungu...ooh..tutengeneze Mnara mpaka mbinguni...tukamchunguze Mungu, meaning wazidi kuchimba mambo kwa umoja watake kumjua Mungu zaidi.Mungu kawachungulia kaona hawa wajinga kwa huu umoja ni threat kabisa..kawavuruga lugha hakuna kuelewana, kawatawanya ulimwenguni kote..meaning...misuguano ikaanza, hakuna kupoa mpaka leo.
MTI WA UZIMA HATUWEZI KAMWE KUULA[TUNDA]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…