Hapo inaonyesha kuwa bastola bado haijafytuliwa, isipokuwa mkono upo kwenye "trigger" huku "barrel" ikiwa imeelekezwa mguuni. La sivyo kama ingalitumika tungaliona alama ya moshi kutoka, damu, na pia ishara ya mtu kugugumia kwa maumivu makali.
Uwepo wa bendara ya Tanzania katika kikaragosi hiki huenda ikawa ni ishara ya dola ya nchi yetu. Miguu ni mhimili mkuu wa mnyama yoyote yule aweze kusimama wima ama imara. Kwa hiyo huyo mtu kujielekezea mwenyewe mtutu mguuni ili kujilipua, ni dalili ya kuwa dola kwa kufanya vitu fulani fyongo inajihatarisha yenyewe ama hata kupelekea anguko lake lenyewe.
Wajuvi watadadavua zaidi.