Mimi nimemuelewa Masoud Kipanya. Wewe je?

Mimi nimemuelewa Masoud Kipanya. Wewe je?

Mama alisema yeye na jiwe walikuwa kitu kimoja.

Akianza kumfukunyua na kumkosoa jiwe ni sawa na kujilipua yeye mwenyewe.

Hao wanaomshauli mazaa wanampoteza ni bora amuache jiwe apumzike yeye apambane kivyake
 
Mtu/binadamu: Ni serikali na nchi ya Tanzania.

Miguu: Ni nguzo aliyoisimamia,ambayo imekosa stara ya viatu ( Ni demokrasia)

Vidole: Ni uongozi wanatakiwa kusimamia/Kubalance hiyo nguzo ya Demokrasia

Kidole kikubwa: Ni kiongozi mkuu mwenye kupambania hiyo nguzo.

Bastola: Ni kinga, matatizo na mazuio ya mambo ya viashiria demokrasia.

Kushushwa kwa Bastola: Ni serikali kutoa vikwazo vya kuimarisha demokrasia bila kusahau kushushwa inaweza kuwa imeelekeza matatizo kwenye vidole hasa kidole kikubwa, ikisubiri kuvuta trigger tuu.
 
Ni kama vile kuna mahali,kwa kauli na Matendo yake,amejilipua mwenyewe badala ya alichokitegemea!
Ebu na nyinyi nisadidieni
[emoji116][emoji116]View attachment 2505550Kipanya anamaanisha Samia anajilipua mwenyewe kwa kudhani kwamba kuiponda Serikali ya Awamu ya Tano kutamuinua kisiasa na hicho ni kiraka kwenye tako la Mama Samia amabcho maana yake ni kwamba yeye aliingia madarakani kama kiraka na siku zote kiraka ni kikara tu hakitageuka kuwa bora.
 
Hapo inaonyesha kuwa bastola bado haijafytuliwa, isipokuwa mkono upo kwenye "trigger" huku "barrel" ikiwa imeelekezwa mguuni. La sivyo kama ingalitumika tungaliona alama ya moshi kutoka, damu, na pia ishara ya mtu kugugumia kwa maumivu makali.

Uwepo wa bendara ya Tanzania katika kikaragosi hiki huenda ikawa ni ishara ya dola ya nchi yetu. Miguu ni mhimili mkuu wa mnyama yoyote yule aweze kusimama wima ama imara. Kwa hiyo huyo mtu kujielekezea mwenyewe mtutu mguuni ili kujilipua, ni dalili ya kuwa dola kwa kufanya vitu fulani fyongo inajihatarisha yenyewe ama hata kupelekea anguko lake lenyewe.

Wajuvi watadadavua zaidi.
Umejitahidi kufafanua Vizuri.
 
Back
Top Bottom