Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naogopa watanichukuliaje?

Njaa haijakupiga hiyo Biashara Nchi zilizoendelea wanafanya watu wenye uwezo mkubwa na unakuta mtu anatumia Ford Ranger kufata nyanya/kabechi shambani wewe nyanya unaweza kuzifata hata kwa Bajaji unalala daah..
 
Watanichukuliaje ni kauli inayoongoza KULAZA NJAA wajinga wajinga nchini.
Nilimaliza degree ya BAF nikaanzisha kituo cha Day care na uji nikapika na watoto wakanikojolea.
 
Sasq kama nilipo wanachuki wanawwza kuniachia nikavitumia mwenyewe
 
ndio umasikini wako huo..

ksms unschukia umasikini huwezi kua hivyo
 
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naona aibu kutoka na mazingira niliyopo na namna watu watanichukulia

Naombe ushauri wenu?
Washawahi kukuletea msosi au pesa ya matumizi ? Vaa ujasiri wiki tu unazoea, au la tafuta eneo la mbali
 
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naona aibu kutoka na mazingira niliyopo na namna watu watanichukulia

Naombe ushauri wenu?
Huna tatizo ndugu!
Tatizo watakuwa nalo wale watakaokusema na kukudharau!
Utapata hela, zaga kwako siyo tatizo, utahudumia jamii, vichenji chenji kwako siyo shida tena, kama una watoto basi hela ya wao kutumia shuleni haitakuwa shida tena. HONGERA. Piga hela ndugu..
 
Sasq kama nilipo wanachuki wanawwza kuniachia nikavitumia mwenyewe
Mwanzoni umesema unaogopa watu watakuchuliaje. Hapa unasema ulipo watu wana chuki na wanaweza kukuachia ukavitumia mwenyewe. Inaelekea zamani ulikuwa na maisha mazuri na ulikuwa ''huna mpango'' na majirani zako, ukajenga chuki na sasa baada ya hali yako kuyumba, unaogopa hata kufungua genge kwa kuogopa watakucheka na kukususia. Solution ni kuhama au kwenda kufungua hilo genge sehemu ya mbali ambako watu hawakujui. Pia acha nyodo na dharau.
 
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naona aibu kutoka na mazingira niliyopo na namna watu watanichukulia

Naombe ushauri wenu?
Kumbe wewe ni matrakoooooo sana sasa watakuchukuliajeee kivip sasa bwege sana wewe
 
Watanichukuliaje ni kauli inayoongoza KULAZA NJAA wajinga wajinga nchini.
Nilimaliza degree ya BAF nikaanzisha kituo cha Day care na uji nikapika na watoto wakanikojolea.
Hizi day care ambazo huku Mwakavuta ada kwa mwaka laki nane kwa mtoto mmoja si ni project ya nguvu ya kuhitaji mtaji na unakua na kipato cha kueleweka 100%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…