Mimi sijawahi kuwa mvuta bangi maisha yangu yote na kama ninavuta mungu ananiona

Mimi sijawahi kuwa mvuta bangi maisha yangu yote na kama ninavuta mungu ananiona

mr gentleman

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2012
Posts
3,222
Reaction score
4,689
Kuna baadhi ya watu ambao huamini kuwa mtu akishakuwa msanii wa muziki ni lazima atakua mtumiaji wavilevi kama bangi, na wapo wanaoamini kuwa binti akishaingia kwenye sanaa ya urembo pia ni lazima atajihusisha na umalaya, kitu ambacho si kweli kwasababu hiyo ni tabia ya mtu binafsi.
Linex Sunday Mjeda leo ameamua kujibu swali ambalo amekuwa akikutana nalo kila mara katika mahojianola kama anavuta bangi ama laa kwasababu ya muonekano wake na pia kuwa msanii.

Kupitia Facebook Linex ameandika:

“Kwa mala ya kwanza Leo nimegoma kujibu swali ambalo nimekua nikiulizwa Sana na vyombo vya habari na swali lenyewe ni kuhusu mimi kujihusisha na matumizi ya uvutaji Bangi. Leo nawambia watanzania na wasio watanzania Mimi sijawahi kua mvuta Bangi maisha yangu yote na Kama nna vuta Mungu ananiona na ningekua mvuta bangi nisingekua na sababu ya kukataa.

Wavuta bangi hamuwasemi hamuwaulizi swali hilo Mimi nisievuta ndo kila siku naulizwa hlo swali narudia tena Sijawahi kua mvuta Bangi sina ratiba ya kutumia dawa za aina yoyote ya kulevya Msinijudge kwa muonekano wangu hivi ndivyo nilivyo na siwezi kua MTU mwingine ‪#‎Sunday‬ Mangu”.

linex-kuhusu-bangi.jpg


 
10639583_10201935370386486_6818940701190849875_n.jpg


10645019_10201740590437109_7882067339731917941_n.jpg


uyu ndio Linex wanaemsingizia kuwa anavuta bange kwa wasio mfaam
 
Nilishangaa nilipomuona Meneja wa Linex kuna mambo ni magumu kuelewa...

watu huwa wanakubali basi siku wakishikwa ndio anabaki mdomo wazi kutafuta excuse
 
Kwani nini bwana Linex si uchome tu na Mungu akuone na watu wakubali kwani bangi si mboga!
 
hahaha, haya ila kwa macho yangu mwaka 2011 nilimshuhudia alikuwa kaja kupiga shoo Dodoma (UDOM).
Kwa wengine ni mboga tu na ni sigara japo mimi situmii lakini sina tabu nao.
 
watu wanasema anavuta sababu mdomo wake umeungua na mweusi kama anachoma nyasi
 
Linex kakaanga mboga sana na kina Dunga na Kunguru wa Nai! Siku wana shoot video ya wimbo wa Mpenzi walipata supply from my source!



Sent from my WhiteBerry using JamiiForums
 
watu wanasema anavuta sababu mdomo wake umeungua na mweusi kama anachoma nyasi
Unajua kuvuta bhangi si tatizo ,tatizo ni kuwa mvuta bhangi! kama vile inavyokuwa si mbaya sana kulewa ila mbaya kuwa mlevi ,au kugegeduka kidogo si tatizo tatizo kuwa mzinifu!
 
Kuandika hajui, sasa kwani akivuta ye avute tu bana kila atafwa kivyake

Dinazarde hivi umeelewa hapo alipoo andika kuwa "kwa Mara ya kwanza nimegoma kujibu swali ambalo nimekuwa nikiulizwa na vyombo vya habari"
halafu kwa chini amejibu!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom