Mimi sio mtoto wa kufikia. (Tafakuri)

Mimi sio mtoto wa kufikia. (Tafakuri)

Habari wakuu!

Wachungaji na makasisi wametufanya tuwe watoto wakufikia. Kama haitoshi Mashekhe na maimamu wametugeuza watoto haramu katika nyumba ya Baba yetu. Wameturubuni kwa maneno ya uongo na hadithi za kutunga. Nasi tumekubali kuishi kama watumwa katika nyumba yetu.

Wamejipa haki ya umiliki wa ukweli. Eti ukweli wa Neno la Baba yetu ambaye wamemfanya kwetu kama Bosi wetu kumbe ni Baba yetu. Si kwamba hawajui yakuwa yeye ni Baba mzazi na mwenye kutulea katika nyumba hii. Na mali zote alituwekea sisi lakini wamemficha hata hatumuoni ili kujilimbikizia mali zake kusudi sisi tuishi kwa taabu katika nyumba yetu.

Eti tukirudi nyumbani tukakuta hakujapikwa tusiulize kwa nini hakujapikwa kisa Baba yetu haulizwi na hapaswi kuulizwa. Je Baba yangu mzazi na mlezi nisimuulize kuhusu chanzo cha njaa yangu, chanzo cha matatizo yangu. Je nikikosa mavazi pia nisimuulize. Mimi sio mtoto wa kufikia nasema. Ninayo haki ya kuuliza yanayonihusu.

Huko Kwenye mahekalu nikiuliza kwa nini Baba yangu aliondoka na kuniacha mkiwa. Nikiuliza kwa nini naumwa, na kupatwa na mikosi kama sio majanga ya kila namna. Naambiwa napaswa kushukuru kwa kila jambo kwani ni mipango ya Baba yangu na ipo siku ataniokoa katika utumwa na taabu zote. Iweje niishi kwa tabu katika nyumba aliyojenga Baba yangu.

Mimi sio mtoto wa kufikia. Ni mtoto halali wa Baba yangu. Nitauliza na kuomba chochote nikitakacho. Nikisema hivi naambiwa namkufuru Baba yangu aliyeenda mbali. Niacheni nimkufuru, yeye ndio anajua namna ya kunishughulikia kama mwanae. Iweje nyie mnisemee na kunichongea kwa Baba yangu.

Mnanipa vitisho eti nitakufa kifo kibaya, eti Baba yangu hadhihakiwi hivyo atanipa fresh ya shamba. Sijajua mnamzungumzia Baba yake nani. Ila kama ni Baba yangu mtasubiri sana. Baba yangu alinipa mali nyie mkanituliza kwa maneno yenu ya hila yenye utamu na huruma ya kiutu.

Mkaniambia nitoe Kodi ambayo mliita sijui zaka na sadaka looh! Hivi tokea lini Mwana akalipa kodi kwenye nyumba ya Baba yake. Mimi sio Mtoto wa kufikia ili nilipe Kodi mliyoiita zaka na sadaka. Baba yangu anamali nyingi sana ndio maana akanijengea nyumba ya kuishi sasa nilipe vipi Kodi.

Mambo yanayomhusu Baba yangu mnajifanya mnayajua sana. Mara Baba yangu yupo Mbinguni, sijui kila mahali, sijiu ana wapambe zake ambao ninyi mliwaita malaika. Mnanichonganisha na Baba yangu eti sifuati taratibu zake. Yeye alinambia kuwa niishi kwa raha mustarehe katika nyumba yake ambayo ni yangu kwa sasa. Lakini mwanifundisha elimu ya kijinga sana.

Mimi sio Mtoto wa kufikia. Eti Kuhoji kama Baba ananipenda au la ni kosa langu. Kwani mimi kujua napendwa ni kosa. Hivi nikipatwa na majanga makubwa na Baba yangu akaniangalia tuu bila kufanya lolote wakati anauwezo wa kuyazuia alafu nikiuliza upendo wa Baba kwangu ninyi mnasema nakufuru tena mnasema nitachomwa na Baba yangu mpenzi.

Nataka niuambie ulimwengu. mimi sio mtoto wa kufikia. Huyu ni Baba yangu. Hizo hadithi za kanisani na kwenye mahekalu. Hadithi za kwenye misikiti na masinagogi msiniambie mimi.
Mnachekesha sana.

Iwafikie wote wenye Baba kama Mimi.

Joka Jeusi ni mtoto wa pekee katika familia ya Baba aliyeenda nchi za mbali. Lakiji anakabiliwa na changamoto ya madalali wanaojifanya wanamjua Baba yake.

Karibuni kwa Mada
Tafuta imani yako. Baki na imani yako. Tafadhali, don't push your FAITH to other people kama Wazungu walivyofanya kwakutusukumia imani zao kwetu ambazo mpk leo zinatutesa...

Km umeona ni mafanikio kutokumwamini "baba" yetu, basi wewe baki na mafanikio yako...usije kwetu kutulazimisha kukubaliana na ww kwamba mafanikio ni kutokumkubali "baba" yetu kama 'baba'.
Nikiamini kama 'baba' yupo nitakufa na nitaoza. Nisipoamini kama 'baba' yupo pia nitakufa na nitaoza. Options zote zinatoa FIXED ANSWER!

DON'T PUSH YOUR FAITH ON ME. YOU'LL BE DISAPPOINTED!
 
Unajua baba ni nani?
 
Inawezekana vp hayo mengine unaona wamebuni ila la kuhusu hiyo Baba ako ndio wanasema sahihi!

Vp ikiwa huyo unaedhani ni Baba ako kumbe sie?
Vp ikiwa huna Baba kabisa au hivyo unavyomdhania Baba hayupo hivyo kabisa? Maana jinsi unavyomfikiria hiyo baba ako alivyo ni kutokana na maelezo yanayoelezwa na hao hao unaowapinga.
 
Sio kila mwanadamu ni mwana wa Mungu, ndio maana kizazi cha kwanza Kaini alimuua nduguyake Abeli. Wana original wa Mungu Baba hawana mashaka nae humuomba na yeye huzisikia Sauti zao. Mleta mada jitathimini upya labda humjui baba yako kwa maana hata Ibilis(joka jeusi la kale) linazaa na wanawake wanadamu na kupata watoto wake ambao ni wanadamu kamili wanaoforce matendo yote maovu yawe huru Kama ushoga, uchangudoa, utoaji mimba, uvivu wa kufikiri, uchawi, kuiba wake za watu n.k. Kwa hiyo nenda kamlilie baba yako
 
Wapi nimempush mtu mkuu?
Huenda Baba yangu si Baba yako
 
Inawezekana vp hayo mengine unaona wamebuni ila la kuhusu hiyo Baba ako ndio wanasema sahihi!

Vp ikiwa huyo unaedhani ni Baba ako kumbe sie?
Vp ikiwa huna Baba kabisa au hivyo unavyomdhania Baba hayupo hivyo kabisa? Maana jinsi unavyomfikiria hiyo baba ako alivyo ni kutokana na maelezo yanayoelezwa na hao hao unaowapinga.

Hata kusingekuwa na Biblia au Quran mtu mwenye akili asingekosa kujua kuwa Yupo Baba. Nenda kwenye jamii zisizotambua dini za watu weupe wao pia huamini Baba yupo. Hivyo madai ya kusema wao ndio wameleta hiyo dhana ni butu na hayana mashiko.

Siwezi dhani Baba yangu siye wakati mimi ndiye, uwepo wangu ni uthibitisho tosha kuwa Yupo Baba yangu.
Nawapinga kwa kunifanya mtoto wa kufikia kiasi kuwa sina uhuru wa kumfikia Baba yangu bila wao jambo ambalo hufanya na watoto wa kufikia
 
Sio kila mwanadamu ni mwana wa Mungu, ndio maana kizazi cha kwanza Kaini alimuua nduguyake Abeli. Wana original wa Mungu Baba hawana mashaka nae humuomba na yeye huzisikia Sauti zao. Mleta mada jitathimini upya labda humjui baba yako kwa maana hata Ibilis(joka jeusi la kale) linazaa na wanawake wanadamu na kupata watoto wake ambao ni wanadamu kamili wanaoforce matendo yote maovu yawe huru Kama ushoga, uchangudoa, utoaji mimba, uvivu wa kufikiri, uchawi, kuiba wake za watu n.k. Kwa hiyo nenda kamlilie baba yako

Baba yangu ndiye aliyemuumba Joka Jeusi la kale na kumpa kusudi la kuwa muasi. Bila Baba yangu hakikufanyika chochote(kiwe kizuri au kibaya) Baba yangu ndiye kila kitu yaani ubaya na wema ndio yeye. Kupewa uhusika wa ubaya au wema ni kusudi tuu lililopo katika mipango yake.

Vitu vyote vinatoka kwake. Hata huyo shetani ni asili ya Baba yangu.
 
Mkuu Mungu nayemjua mimi kamwe kamwe hawezi kumchoma kiumbe chake aliyekiumba mwenyewe kwa udhaifu kama huu..ila watu wa dini wametuamisha ivyo.God is love!

Baba yangu wamemfanya kitu cha hatari kuliko shetani
 
Hoja ni ya kufikirisha sana. Kuna ndugu zetu pia,ndugu zetu kabisa wa damu wamejiita baba ,yaani wanatutisha,wanasema wakiamua jambo ,baba analibariki,hao ambao wanajiita baba sisi ndio tunawalisha kwa kodi zetu. Wanadai wako sawa na baba kabisa,lakini mbona ni wakatili ,na wanadai wakipenda wanaweza kukupandisha daraja ukawa kama wao. Hata ukifa wanaweza fanya namna Fulani ukapanda cheo. Wengine ni marehemu na wakati wapo nasi wakatuagiza tukitaja jina lao tumalizie na kibwagizo cha kuwambea kwa baba. Kwa kweli kuna maajabu sana

Baba yangu Baada ya kwenda safari za mbali na kutuachia mimi na ndugu zangu nyumba hii, baadhi ya ndugu hasa waliotutangulia walituhadaa na kuturubuni. Kisha wakasema maneno ya uongo yenye kutufarakanisha na kututenga kimakundi makundi
 
JOka jeusi baba yake atakuwa joka jeusi tiiiiiiiiiiii - baba yako yuko kuzimu mfuate huko huko; hapa duniani ni milki ya wanadamu. Tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge; minyororo ya shetani (joka jeusi tiiiii) imeshindwa!

Sawa Mkuu nitaenda kuzimu huko unapopasemea lakini tambua huko ndiko asili ya kila mwenye pumzi. Huko ndiko kwetu hapa ni wasafiri tuu. Ukija huko utaelewa kwa nini dunia ilikuwa tupu tena ukiwa huku giza likitawala uso wa dunia na roho ya Baba yangu ikitawala. Baba yangu ukija huku utamuona na utamsalimia Shikamoo naye atakujibu Marhaba
 
Ukishaelewa habari ya jumla kwamba baba Mungu (mjuzi wa yote, mwenye uwezowote na upendo wote) kuwepo ni uzushi tu, hizi stories nyingine za rejareja hazitakusumbua.

Mkuu Amini Usiamini, Baba yangu yupo na hata kabla ya hizo stori za reja reja zenye ubinafsi, ukabila na utaifa. Stori zilizombinafsha Baba yangu na kumuita Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Stori zilizomtaifisha Baba yangu na kumuita Mungu wa Israel jambo ambalo ni mwamba ngoma huvutia kwake. Ndilo linakufanya usiamini uwepo wa Baba yangu.

Ila utakapo kufa ndipo utakapoamka
 
Thibitisha yupo na si stories tu.

Maana inawezekana unakataa uongo wa Mungu wa Ibrahimu, na kukubali uongo mwingine

Unajuaje unachoamini si uongo?
 
Back
Top Bottom