DOKEZO Minada ya mali chakavu za serikali inayofanywa na watumishi wa serikali au wahakiki mali ichunguzwe

DOKEZO Minada ya mali chakavu za serikali inayofanywa na watumishi wa serikali au wahakiki mali ichunguzwe

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

HAKI KWA WOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
2,783
Reaction score
2,396
Habarini,
Mida ya mali chakavu za Serikali zinazouzwa kama vile fenicha, magari n.k imekuwa ikifanywa na Watumishi wa Serikali na mhakiki mali ambao kiuhalisia wanaleta urasimu mkubwa kwenye fedha zinazopatikana kwa maslahi yao hasa kwa upande wa magari.

Inakuwaje watumishi na wahakiki mali ndiyo wasimamie hiyo minada wakati kuna madalali waliosajiliwa Wizara ya Fedha na wanalipia leseni za udalali kutoka Hazina na leseni za biashara kutoka halmashauri?

Hii tabia ndiyo inafanya wananchi waichukie Serikali kwa kuwa Watumishi wa Serikali wamebana kila eneo kuanzia ajira maofisi na bado wanataka hata kazi za minada wafanye wao kitu ambacho ni roho mbaya.

Minada inafanyika mezani kabla ya tarehe husika na pesa nyingi zinaingia mifukoni mwao huku serikali ikipata kiasi kidogo sana.

Hao TAKUKURU wapo tu wala hawalioni hili na kufuatilia rushwa zinavyofanyika kwenye minada ya mali za Serikali hasa Polisi na Halmashauri kumekithiri haya mambo lakini TAKUKURU wanaangalia tu hivi wanashindwa kufuatilia na kunusa mali zimeuzwa kiasi gani na je fedha zilizolipwa ndizo zilizoingia serikalini kama siyo zimeenda wapi?

Madalali wanalipia leseni na kodi kila mwaka lakini Watumishi wa Serikali wanashikiria kila mnada wa Serikali manake nini kama siyo ujinga?

Viongozi wapo tu wanaangalia WAHAKIKIMALI chakavu za Serikali wanapiga dili tu, iweje WAHAKIKIMALI wafanye kazi ya kuhakiki na haohao wauze hizo mali na kusinamia minada ya serikali wakati kuna makampuni yana leseni za uDALALI hawana kazi ?

Ukiwauliza WAHAKIKIMALI au HAZINA wanadai MADALALI wanapiga hela 10% hivyo Serikali inakosa hela kwahiyo wao ndiyo wanachukua hiyo 10% sasa na bado wana mishahara n.k.

Mambo kama haya ndiyo hufanya watu wakose vipato na kujenga chuki kwa Serikali na viongozi wake.
 
Ujangiri ni mwingi sana nchini.

20251129_033814.jpg


InaumaSana/ItHasAForkVery
 
Habarini,
Mida ya mali chakavu za serikali zinazouzwa kama vile fenicha,magari,nk imekuwa ikifanywa na watumishi wa serikali na mhakiki mali ambao kiuhalisia wanaleta urasmu mkubwa kwenye fedha zinazopatikan kwa maslahi yao hasa kwa upande wa magari.

Inakuwaje watumishi na wahakiki mali ndiyo wasimamie hiyo minada wakati kuna madalali waliosajiriwa wizara ya fedha na wanalipia leseni za udalali kutoka hazina na leseni za biashara kutoka halmashauri?

Hii tabia ndiyo inafanya wananchi waichukie serikali kwa kuwa watumishi wa serikali wamebana kila eneo kuanzia ajira maofisi na bado wanataka hata kazi za minada wafanye wao kitu ambacho ni roho mbaya.

Minada inafanyika mezani kabla ya tarehe husika na pesa nyingi zinaingia mifukoni mwao huku serikali ikipata kiasi kidogo sana.

Hao WAJINGA TAKUKURU wapo tu wala hawalioni hili na kufuatilia rushwa zinavyofanyika kwenye minada ya mali za serikali hasa polisi na halmashauri kumekithiri haya mambo lakini TAKUKURU wanaangalia tu hivi wanashindwa kufuatilia na kunusa mali zimeuzwa kiasi gani na je fedha zilizolipwa ndizo zilizoingia serikalini kama siyo zimeenda wapi?

Madalali wanalipia leseni na kodi kila mwaka lakini watumishi wa serikali wanashikiria kila mnada wa serikali manake nini kama siyo ujinga?

Viongozi wapo tu wanaangalia WAHAKIKIMALI chakavu za Serikali wanapiga dili tu,iweje WAHAKIKIMALI wafanye kazi ya kuhakiki na haohao wauze hizo mali na kusinamia minada ya serikali wakati kuna makampuni yana leseni za uDALALI hawana kazi ?

Ukiwauliza WAHAKIKIMALI au HAZINA wanadai MADALALI wanapiga hela 10% hivyo serikali inakosa hela kwahiyo wao ndiyo wanachukua hiyo 10% sasa na bado wana mishahara n.k.

Mambo kama haya ndiyo hufanya watu wakose vipato na kujenga chuki kwa serikali na viongozi wake
hawa jamaa wahuni sana wanauziana wenyewe kwa Bei chee

Hawana huruma na hili taifa
 
hawa jamaa wahuni sana wanauziana wenyewe kwa Bei chee

Hawana huruma na hili taifa
Sasa nauliza TAKUKURWA wana kazi gani hawa ******* mali za serikali zinaharibiwa na kuuziana kila kukicha siku mbili tu baada ya mnada unaziona barabarani wanazo watumishi,viongozi wa serikali,wanasiana au ndugu zao na wamenunua kwa bei rahisi tu,kivipi?
 
Back
Top Bottom