Mining ni pesa isiyo na jasho

Refrector

Senior Member
Joined
Mar 13, 2014
Posts
187
Reaction score
118
Jamani watanzania tuamke Dunia inaenda mbio sana. Kama utang'ang'ana na biashara moja hakika kilio kwako kiuchumi kitakusonga hivyo jifunze kujivunia pesa mtandaoni kama wenzako wanavyofanya.

Kwanini bando lako liwe la kufacebuka tu na kuwasapika tuu bila kuingiza hata mia...

Shituka ingia Dunia ya wapambanaji ujue walau kuingiza hata $50 tu ya mdhungu.😁

Kuna pesa nyingi mtandaoni lakini Anza na hizi ambazo huwekezi hata mia yako mtandaoni... Mining, Freelancing, gathering coin nk

Ukishakuwa mwenyeji mtandaoni ndio jiingize kwa hao Forex na wengineo....

Huku kunavitu vingi vya kufanya na kujiingizia pesa kikubwa ni kumpata mtu sahihi na asiye na tamaa ya kukuomba pesa akuelekeze...

Vijana changamka pesa ya mtandao ipooo👌Wakenya wanapiga pesa, Nigerian, Uganda na nchi za west kwanini sisi Tuwe mikia Kila sehemu🥴

Ni hayoo tuu niloyaleta Leo kama utahitaji kujua usisite kuniinbox 🙏
 
Toa mbinu, usije ukawa unauza tu hizo mbinu inbox. Tuinuane hapa hapa nipo tayari kujifuza.
 
Unaonaje kama utaanzisha darasa hapa
 
Umeishia kulalamika tu bila ku-come up na elimu hata shikizi...umefanya uzi wako uwe uselessly!!
 
Mkuu hizo GPU card uwezo wa kuzinunua tunao kweli, maana GPU moja ya kusupport mining ni kati ya tsh400,000 na ili uone faida zinatakiwa zaid ya 3, yan had umekamilisha mining rig unajikuta ume invest kama 4milion, hapo bado pc yenye processing power kubwa...... SO MINING SIO PESA YA BURE TU KAMA UNAVYOIELEZEA.... ni investment..
 
Mtanzania kuanzia mastaa uchawara wetu mpaka mtu wa kawaida wanachukulia mitandao ya kijamii kama sehemu ya umbea, hawajuwi lolote.
 
Mto maada anataka kuingiza watu chaka. In short hakuna pesa ya bure. Na ogopa mtu anaye kushawishi kwamba kuna pesa mahali ni ya kuchukua tu.
 
Mkuu Hii mada yako si ungeianzisha huko inbox?
 
2
Mtu akimudu hizo ghalama za uwekezaji, kuna ka faida kweli?
 
Mining zipo za aina nyingi na kama unahitaji kuzijua za Bure zipo pia nyingi Sana na ni jinsi tu ya kuoneshwa hii fanya hii acha...kifupi uwe na mjuvi wa haya mambo usikurupuke🤗

Mm nilikuwa kama ww nahofia pesa yangu but nikamwambia alonielekeza hii kitu kama ni ya kuwekeza pesa mm sintaiweza alichoniambia ni kuwa uwe na moyo wa uvumilivu maana nyingine inachukua muda wa miezi 6 na zaidi nikaona kuhusu kusubiri sio issue but mbaka naandika huu Uzi nimeonja matunda yake tr.16 January hii👌
 
Tupate majibu hapa
Kwa sasa mfano kumine bitcoin bila minning plant na jinsi ya kupata umeme wa bei rahisi gharama za umeme zitazidi unachopata. Ndio maana miners wengi ama ni wezi wa umeme, au wamefunga mifumo ya uchimbaji na wanazalisha umeme kutumia maji wenyewe.
 
Mtanzania kuanzia mastaa uchawara wetu mpaka mtu wa kawaida wanachukulia mitandao ya kijamii kama sehemu ya umbea, hawajuwi lolote.
Inawezekana wewe ndio hujui lolote huohuo umbea ndio unawaingizia pesa kupitia hiyo mitandao.

Japo mada haihusian na kupiga pesa kwenye mitandao ya kijamii.
 

Unazungumzia mining zile ukitaka kuWithdraw coin zako, unaambiwa mpaka ulipie maintanance fee?... Jau sana zile.... nimeshazifanya nyingi sana , bila kutoa hela kidogo ili uongezewe Hash, hakuna faida utaiona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…