Minnesota Mji Uliojaa Wasomali, Kiasi cha kuhatarisha Usalama wa Marekani, Trump Awapelekea Moto

Mhaya

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2023
Posts
2,818
Reaction score
7,940
Kwa sasa kuna mvutano mkubwa Minnesota kati ya jamii ya Wasomali (ambayo ni karibu 80,000 wenye asili ya Kisomali) na serikali ya shirikisho na ya jimbo. Hii imetokana na madai madhubuti ya udanganyifu mkubwa wa fedha za umma pamoja na hatua za Rais Donald Trump kuongeza ukaguzi wa uhamiaji na kuondoa ulinzi wa kisheria uliokuwa unawalinda wakimbizi hao.

Jamii ya Wasomali ilianza kuja Minnesota miaka ya 1990 kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Somalia. Tangu wakati huo idadi yao imeongezeka haraka na sasa Minnesota ina mojawapo ya jamii kubwa zaidi za Wasomali Marekani.

1. Makosa yanayodaiwa kutendwa na Wasomali katika eneo hilo

Uhusiano na Ugaidi:
Kuna madai kuwa sehemu ya fedha zinazopolwa hapo Minnesota zimepelekwa Somalia kupitia mfumo wa hawala na kufikia makundi kama Al-Shabaab. Uchunguzi unaendelea lakini bado hakuna kiasi kilichothibitishwa. Kauli hizi zimemfanya Trump kutoa matamshi makali dhidi ya Wasomali na kusema “wameharibu nchi yetu na wanafadhili ugaidi nchini kwao.”

Udanganyifu wa kifedha kupitia feeding our future: Tangu 2020 maafisa wa shirikisho wamesema jamii ya Wasomali imehusishwa na udanganyifu mkubwa wa programu za serikali, hasa wakati wa COVID-19. Shirika la Feeding Our Future ambalo limekuwa likisimamiwa na Watu wa jamii ya Kiislamu hasa Wasomali lilidaiwa kuiba zaidi ya dola milioni 250 kupitia madai ya uwongo kuhusu misaada ya milo ya watoto kwa kulaghai karatasi za malipo, kujaza taarifa za uongo na kuongeza majina na takwimu hili kujiongezea pesa hizo za misaada.. Zaidi ya watu 59 wamehukumiwa na uchunguzi wa zaidi ya dola bilioni 1 unaendelea. Hii imehusisha udanganyifu wa madai ya huduma za chakula, matibabu na huduma za nyumbani. Kujipatia pesa kwa njia za kugushi takwimu na taarifa.

Udanganyifu wa Autism na Medicaid: Medicaid ni mpango wa afya na bima ya matibabu inayotolewa na jimbo huko Marekani kwa watoto, wajawazito, watu wenye kipato cha chini, wazee wenye uhitaji, watu wenye ulemavu, na watu wenye kuhitaji huduma maalumu hasa wenye magonjwa au shida zenye kuhitaji huduma ya muda mrefu kama wagonjwa wenye usonji (Autism) na kadharika, lengo ni kurahisha matibabu, ununuzi wa dawa. Zaidi ya kliniki 85 za autism zinazoendeshwa na Wasomali zinachunguzwa kwa madai ya udanganyifu wa Medicaid yanayofikia dola milioni 399 mwaka 2023.

Kuna kesi ambapo shirika la tiba lililokuwa linadai kutoa huduma kwa watoto wenye autism — Smart Therapy — limekabiliwa na mashtaka ya “wire fraud” kwa madai ya kupokea pesa kutoka Medicaid bila kutoa huduma halisi.

Maandishi ya korti yanabainisha kuwa huduma kama tiba, usafirishaji wa watoto, chakula (meals) n.k — zilidhinishwa kwenye madai (invoices) — lakini katika vitendo hizi huduma hazikuwahi kutolewa, au zilionekana kuwa “bogus”: magari ya kuchukua watoto, waraka wa kuhudhuria, “attendance roster”, orodha ya chakula/meal count — vyote hivyo viliandaliwa ili kuhalalisha madai ya reimbursement.

Wadau kadhaa — watoa huduma — walikuwa na “staff/watendaji” wasio na ujuzi maalum wa matibabu ya autism (wasio na sifa, mafunzo, au hata cheti cha kuruhusiwa) — hivyo huduma zilizodaiwa hazikuwa na msingi wa kitaalamu.

Pia kuna madai ya “kickbacks” — yaani, wazazi wa watoto walipewa pesa — kila mwezi, kadiri watoto walivyoingia/kupokea huduma — ili wapate kusajili watoto wao na kupata huduma kupitia Smart Therapy.

Kwa muhtasari — hizi ndio mbinu ambazo watekelezaji wa udanganyifu walitumia: Kuchapisha “invoices” / madai ya reembolso kwa huduma za autism, usafirishaji, chakula, n.k — hata wakati huduma hao hawakutolewa. Kutumia “staff” wasio na sifa — mara nyingi wa umri mdogo, au hao ambao hawakufanya kazi halisi — ili kufanya utoaji wa huduma haramu kuonekana halali. Kuwapa wazazi “kickbacks” (malipo ya kila mwezi) kama motisha ya kusajili watoto — hivyo kutumia familia kama sehemu ya wito la udanganyifu. Kuandaa nyaraka bandia, waraka wa kuhudhuria (“attendance roster”), orodha za chakula, na “signatures/approvals” za watu ambao hawakuhudumia — vilevile “mashirika ya utumaji chakula/meal vendors” bandia — ili kulipia kama ilivyokuwa halisi.

2. Hatua za Rais Trump na Uhamiaji

Trump ameanzisha operesheni maalum Minnesota inayolenga jamii ya Wasomali. Zaidi ya maafisa 100 wa ICE wanatumika kuwakamata wale wenye amri za kufukuzwa (Wahamiaji haramu). Mwaka 2025 alitangaza kumaliza hadhi ya muda ya ulinzi (Temporary Protected Status) kwa Wasomali 705 wa Minnesota, akidai uwepo wa “makundi ya wavamizi.”

Hatua hii imesababisha hofu katika jamii. Wawakilishi wa Wasomali wanasema inazidisha chuki dhidi ya wahamiaji. Hata hivyo takribani 80% ya Wasomali Minnesota ni raia au wenye vibali halali.

3. Maoni ya Jamii ya Wasomali na Wakosoaji

Jamii ya Wasomali inachangia zaidi ya dola milioni 500 kwa uchumi wa Minnesota na hulipa zaidi ya dola milioni 67 katika kodi. Wengi wanafanya kazi katika afya, huduma za wazee, na sekta za elimu. Viongozi kama Ilhan Omar wanasema jamii hii ni sehemu muhimu ya muundo wa jimbo.

Gavana Tim Walz na Meya wa Minneapolis Jacob Frey wanapinga hatua za Trump wakizitaja kuwa chuki dhidi ya wageni. Polisi wa Minnesota wamekataa kushirikiana na ICE kuwakamata Wasomali wanaosadikika kuwa ni wahamiaji haramu.

Katika mitandao ya kijamii mjadala ni mkali—baadhi ya Wasomali wanasisitiza hawatatoka Minnesota, huku wakosoaji wakisisitiza kufukuzwa kwa waliohusika waliofanya udanganyifu. Mgawanyiko upo kati ya wanaoona udanganyifu kama tatizo la kikundi cha Wasomali na wanaoona hatua za serikali kuwa ubaguzi.

4. Historia na Muktadha

Jamii ya Wasomali Minnesota ilikua haraka tangu miaka ya 1990. Pia kumekuwa na historia ya changamoto kama kujiunga kwa vijana zaidi ya 20 na Al-Shabaab au ISIS kati ya 2007–2015, pamoja na makosa madogo ya kodi na uhamiaji.

Uchunguzi unaonesha udanganyifu mwingi ulitokea chini ya uongozi wa Mayor wa sasa Bwana Walz tangu 2019. Wakosoaji wanasema serikali ya Minnesota ilikosa ukali ili kuepuka tuhuma za ubaguzi, kitu kilichosababisha hasara ya zaidi ya dola bilioni 1 kwa walipa kodi.


View: https://youtu.be/98hRUchOM4I?si=KnHwbJRXH24x0zjX
 
wasomali wa jinga kama ushapewa uraia si utulie sasa uko marekani bado unagombea ubunge ila bado unalibendera la somalia sasa uraia wa nini si urudi somalia
Wasomali wapo daslm na biashara kubwa hadi Zambia mzee huko SA wana eneo lao Forsburg kabisaa na wana uchumi mkubwa endeleeni kuwatukana mitandaoni wakati wao wanajua wanachokifanya na wakifika kitu cha kwanza ni kuwa Rais kwa kutumia pesa zao kisheria..
 
Hata wale walio kuwepo kitwe na ndola walitengeneza himaya yao kwenye Farm huko hakuna mtu anaweza kuwasogelea, na walifanya kitu Zambia nzima wakashikilia biashara ya Tanks Trucks za mafuta, ukiangalia kwa ustawi wa nchi sidhanii kama ni sawa maana wakipata pesa kweli wanapeleka kwao kuendesha mambo yao ambayo yanazidi kuleta vita tu siku hadi siku, basi wangejaribu kutuliza vita kwao sidhani kama watu wangewalalamikia. Michango inayo kwenda kwao inaendelezaga moto tu, ukifika Garisa utaamini.
 
Siyo wasomali ni waislamu bull.shit
 
Ujawahi kujiuliza kwa nini wasomali wengi wanabiashara kubwa sana maneo mengi hapa afrika.

Hii code na kufungulia,pale kariakoo mtaa mmoja unanguvu kuliko hata serikali ya tz.Pale unapata USD kiasi unachotaka chochote.
 
Mkuu wasomali wakitoka kwao wametoka ni wachache sana wanawaza kurudi home mara nyingi wanatuma hela kuwachukua waliobaki wasomali waliopo nje hawawazi kurudi home na ndio wanafanya biashara ya kutuma pesa popote Duniani na niwaaminifu.
 
Hayo ndo madhara ya kuchoma kwako....kila Kona unakataliwa
 
Jaribu kuangalia vizuri majina unaweza ukakuta yule kigogo was tz yumo
 
Wako smart ila wameshindwa kuweka usumart huo nchini mwao, ni wabinafsi
 
Tatizo ni hiyo dini, inawafanya wawe waongo waongo maana dini inaruhusu uwongo, na wanazaliana sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…